Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Luka 7:2 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

2 Na mtumishi wa akida mmoja alikuwa hawezi, karibu kufa, nae ni mtu aliyependwa nae sana.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

2 Huko kulikuwa na jemadari mmoja ambaye alikuwa na mtumishi wake aliyempenda sana. Huyu mtumishi alikuwa mgonjwa karibu na kufa.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

2 Huko kulikuwa na jemadari mmoja ambaye alikuwa na mtumishi wake aliyempenda sana. Huyu mtumishi alikuwa mgonjwa karibu na kufa.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

2 Huko kulikuwa na jemadari mmoja ambaye alikuwa na mtumishi wake aliyempenda sana. Huyu mtumishi alikuwa mgonjwa karibu na kufa.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

2 Mtumishi wa jemadari mmoja Mrumi, ambaye bwana wake alimthamini sana, alikuwa mgonjwa sana karibu na kufa.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

2 Mtumishi wa jemadari mmoja wa Kirumi, ambaye bwana wake alimthamini sana, alikuwa mgonjwa sana karibu kufa.

Tazama sura Nakili




Luka 7:2
24 Marejeleo ya Msalaba  

Bassi yule akida, nao walio pamoja nae wakimwangalia Yesu, walipoliona tetemeko la inchi na mambo yaliyofanyika, wakaogopa sana, wakinena, Hakika huyu alikuwa Mwana wa Mungu.


Akida alipoona lililokuwa, akamtukuza Mungu, akisema, Kwa kweli mtu huyu alikuwa mwenye haki.


ALIPOKWISHA kuyamaliza maneno yake yote masikioni mwa watu akaingia Kapernaum.


Aliposikia khabari za Yesu akatuma baadhi ya wazee wa Wayahudi kwake, akimwomba aje, amwokoe mtumishi wake.


kwa sababu ana binti, mwana wa pekee, umri wake amepata miaka thenashara, nae yu katika kufa. Na katika kwenda kwake makutano wakamsonga.


PALIKUWA na mtu Kaisaria, jina lake Kornelio, akida wa kikosi kilichoitwa Kiitaliano,


Na yule malaika aliyesema nae akiisha kuondoka, Kornelio akaita watumishi wawili wa nyumba yake, na askari mmoja, mtu mtawa, katika wale waliomkhudumia daima:


Yule akida aliposikia, akaenda akamwarifu yule jemadari, akisema, Unataka kufanya nini? kwa maana mtu huyu ni Mrumi.


Paolo akamwita akida mmoja, akasema, Mchukue huyu kwa jemadari; maana ana neno la kumwarifu.


BASSI ilipoamriwa tusafiri hatta Italia, wakamtia Paolo na wafungwa wengine katika mikono ya akida mmoja, jina lake Yulio, wa kikosi cha Augusto.


Siku ya pili tukawasili Sidon; Yulio akamfadhili sana Paolo akampa rukhusa kwenda kwa rafiki zake, kutunzwa nao.


Bali akida, akitaka kumponya Paolo, akawazuia, wasifanye kama walivyokusudia, akawaamuru wale wawezao kuogelea wajitupe baharini, wafike inchi kavu;


Ninyi watumwa, watiini wao ambao kwa niwili ni bwana zenu, katika mambo yote, si kwa utumwa wa macho, kama wajipendekezao kwa wana Adamu, bali kwa unyofu wa moyo, mkimeha Mungu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo