Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Luka 7:16 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

16 Khofu ikawashika wote, wakamtukuza Mungu, wakisema, Nabii mkuu ametokea kwetu: na Mungu amewajilia watu wake.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

16 Watu wote walishikwa na hofu, wakawa wanamtukuza Mungu wakisema, “Nabii mkuu ametokea kati yetu. Mungu amekuja kuwakomboa watu wake.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

16 Watu wote walishikwa na hofu, wakawa wanamtukuza Mungu wakisema, “Nabii mkuu ametokea kati yetu. Mungu amekuja kuwakomboa watu wake.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

16 Watu wote walishikwa na hofu, wakawa wanamtukuza Mungu wakisema, “Nabii mkuu ametokea kati yetu. Mungu amekuja kuwakomboa watu wake.”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

16 Watu wote wakajawa na hofu ya Mungu, nao wakamtukuza Mungu wakisema, “Nabii mkuu ametokea miongoni mwetu. Mungu amekuja kuwakomboa watu wake.”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

16 Watu wote wakajawa na hofu ya Mungu, nao wakamtukuza Mungu wakisema, “Nabii mkuu ametokea miongoni mwetu, Mungu amekuja kuwakomboa watu wake.”

Tazama sura Nakili




Luka 7:16
31 Marejeleo ya Msalaba  

hatta makutano wakastaajabu, walipowaona bubu wanasema, vilema wanakuwa wazima, viwete wanakwenda, na vipofu wanaona; wakamtukuza Mungu wa Israeli.


Makutano wakanena, Huyu ni Yesu, yule nabii wa Nazareti ya Galilaya.


Wakaondoka upesi kutoka kaburini, kwa khofu na furaha nyingi, wakaenda mbio kuwapasha wanafunzi wake khabari.


Makutano wakimwona, wakastaajabu, wakamtukuza Mungu, aliyewapa watu mamlaka ya jinsi hii.


Khofu ikawaingia wote waliokaa karibu nao; yakaenea maneno haya pia milimani mwote Uyahudi.


Atukuzwe Bwana, Mungu wa Israeli; Kwa kuwa amewajia watu wake na kuwakomboa.


watakuangusha chini, na watoto wako ndani yako; wasikuachie jiwe juu ya jiwe; kwa kuwa hukujua majira ya kujiliwa kwako.


Wachungaji wakarudi, wakimtukuza Mungu na kumhimidi kwa mambo yote waliyosikia, na waliyoona, kwa namna waliyoambiwa.


Akawaambia, Mambo gani? Wakamwambia, Mambo ya Yesu Mnazareti, aliyekuwa mtu nabii mwenye nguvu kwa tendo na kwa neno mbele za Mungu na watu wote;


Ushangao ukawashika wote wakamtukuza Mungu: wakajaa khofu, wakinena, Tumeona maajabu leo.


Simon Petro alipoona haya, akaanguka magotini pa Yesu, akasema, Toka kwangu, kwa sababu mimi ni mtu mwenye dhambi, Bwana.


Yule maiti akaketi, akaanza kusema. Akampa mama yake.


Yule Farisayo aliyemwalika, alipoona haya akasema kimoyomoyo, akinena, Mtu huyu kama angekuwa nabii, angalimjua huyu ni nani! na ni mwanamke gani anaemgusa, ya kuwa ni mwenye dhambi.


Na watu wote wa inchi ya Wagadarene iliyo kando kando wakamwomba aondoke kwao, kwa sababu walishikwa na khofu nyingi; bassi akakiingia chombo akarudi.


Wakajibu, wakasema, Yohana Mbatizaji: na wengine, Eliya: na wengine kwamba nabii mmoja katika wale wa kale amefufuka.


Wakamwuliza, Nini bassi? U Eliya wewe? Akanena, Mimi siye. Wewe u nabii yule? Akajibu, La.


Wakamwuliza, wakimwambia, Mbona bassi wabatiza, kama wewe si Kristo, wala Eliya, wala nabii yule?


Yule mwanamke akamwambia, Bwana, naona ya kuwa u nabii.


Bassi watu wale, walipoiona ishara aliyoifanya Yesu, wakasema, Huyu hakika ni nabii yule ajae ulimwenguni.


Kukawa matangukano kati yao. Bassi wakamwambia yule kipofu marra ya pili, Wewe unasema nini katika khabari zake kwa kuwa alikufumbua macho? Akasema, Yu nabii.


Anania aliposikia maneno haya akaanguka, akafa. Khofu nyiugi ikawapata watu wote walioyasikia haya.


Musa huyo ndiye aliyewaambia wana wa Israeli, Bwana Mungu wenu atawainulieni nabii katika ndugu zenu, kama mimi: mtamsikia huyo.


Wakamtukuza Mungu kwa ajili yangu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo