Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Luka 7:13 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

13 Na Bwana alipomwona, akamhurumia, akamwambia, Usilie.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

13 Bwana alipomwona mama huyo akamwonea huruma, akamwambia, “Usilie.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

13 Bwana alipomwona mama huyo akamwonea huruma, akamwambia, “Usilie.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

13 Bwana alipomwona mama huyo akamwonea huruma, akamwambia, “Usilie.”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

13 Bwana Isa alipomwona yule mjane, moyo wake ulimhurumia, akamwambia, “Usilie.”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

13 Bwana Isa alipomwona yule mjane, moyo wake ulimhurumia, akamwambia, “Usilie.”

Tazama sura Nakili




Luka 7:13
36 Marejeleo ya Msalaba  

Nawahurumia makutano kwa sababu yapata siku tatu wamekaa nami, wala hawana kitu cha kula:


BASSI baada ya mambo haya Bwana akachagua wengine sabaini, akawatuma wawili wawili wamtangulie kwenda killa mji na pahali atakakokwenda mwenyewe.


IKAWA alipokuwa mahali fullani, anasali, alipokoma, mmoja katika wanafunzi wake akamwambia, Bwana, tufundishe sisi kusali kama Yohana alivyowafundisha wanafunzi wake.


Bwana akamwambia, Sasa ninyi Mafarisayo mwasafisha kikombe na sabani kwa nje, lakini ndani yenu mmejaa unyangʼanyi ua uovu.


Bwana akasema, Nani, bassi, aliye wakili mwaminifu niwenye busara, ambae Bwana wake atamweka juu ya ntumishi wake wote, awape watu posho lao kwa saa yake?


Bassi Bwana akamjibu, akasema, Ewe mnafiki, killa mmoja wenu je! hamfungui ngʼombe wake au punda wake mazizini siku ya sabato, akaenda nae kumnywesha?


Mitume wakamwambia, Bwana, utuongezee imani yetu.


Bwana akasema, Mkiwa na imani kama punje ya kharadali, mngeuambia mzambarau huu, Ngʼoka ukapandwe baharini, nao ungewatiini.


Bwana akasema, Sikieni asemavyo yule kadhi asiye haki.


Zakkayo akasimama, akamwambia Bwana, Bwana, nussu ya mali zangu ninawapa maskini; na kama nimetoza mtu kitu kwa kumsingizia uwongo ninamrudishia marra nne.


Bwana akageuka, akamtazamisha Petro: Petro akalikumbuka neno la Bwana, jinsi alivyomwambia, Kabla hajawika jogoo leo, utanikana marra tatu.


Wakaingia, wasiuone mwili wa Bwana Yesu.


wakisema, Hakika Bwana amefufuka, amemtokea Simon.


Bassi, alipokaribia lango la mji, hapo palikuwa na maiti anachukuliwa nje, mwana pekee wa mama yake, nae mjane; na watu wa mji wengi pamoja nae.


Akaenda karibu, akaligusa jeneza; wale wachukuzi wakasimama. Akasema, Kijana, nakuambia, Ondoka.


Yohana akaita wawili katika wanafunzi wake akawapeleka kwa Yesu, akisema, Wewe ndiye yule ajae, au tumtazamie mwingine?


Akasema, Msilie; kwa maana hakufa, bali amelala usingizi.


Ni Mariamu yule aliyempaka Bwana marhamu, akamfuta miguu yake kwa nywele zake, ambae ndugu yake Lazaro alikuwa hawezi.


Bassi wale maumbu wakatuma ujumbe kwake, wakisema, Bwana, yeye umpendae hawezi.


Nao wakamwambia, Bibi, unalilia nini? Akawaambia, Kwa sababu wamemwondoa Bwana wangu, wala sijui walikomweka.


Yesu akamwambia, Bibi, unalilia nini? Unamtafuta nani? Yeye, akidhani ya kuwa ni mtunza bustani, akamwambia, Bwana, kama umemchukua wewe, niambie ulipomweka, nami nitamwondoa.


BASSI Bwana alipojua ya kuwa Mafarisayo wamesikia kwamba Yesu anafanya wanafunzi wengi kuliko Yohana, na kubatiza,


(lakini mashua nyingine zilikuja kutoka Tiberia karibu na pahali pale walipokula mikate, wakati Bwana aiiposhukuru);


na wale waliao kama hawalii; na wale wafurahio kama hawafurahi: na wale wanunuao, kama hawana kitu.


Lakini, ndugu, hatutaki msijue khabari zao waliolala, msije mkahuzunika kama na wengine wasio na matumaini.


Kwa hivyo ilimpasa kufananishwa na ndugu zake katika mambo yote, apate kuwa kuhani mkuu mwenye rehema, mwaminifu katika mambo ya Mungu, illi afanye suluhu kwa dhambi za watu wake.


Kwa kuwa hatuna kuhani mkuu asiyeweza kuyachukua mambo yetu ya udhaifu; bali yeye alijuribiwa sawa sawa na sisi katika mambo yote, bila dhambi.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo