Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Luka 7:12 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

12 Bassi, alipokaribia lango la mji, hapo palikuwa na maiti anachukuliwa nje, mwana pekee wa mama yake, nae mjane; na watu wa mji wengi pamoja nae.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

12 Basi, alipokuwa anakaribia lango la mji, walitokea watu wamebeba maiti ya mwanamume mmoja, mtoto wa pekee wa mama mjane. Watu wengi wa mji ule walikuwa pamoja na huyo mama.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

12 Basi, alipokuwa anakaribia lango la mji, walitokea watu wamebeba maiti ya mwanamume mmoja, mtoto wa pekee wa mama mjane. Watu wengi wa mji ule walikuwa pamoja na huyo mama.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

12 Basi, alipokuwa anakaribia lango la mji, walitokea watu wamebeba maiti ya mwanamume mmoja, mtoto wa pekee wa mama mjane. Watu wengi wa mji ule walikuwa pamoja na huyo mama.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

12 Alipokaribia lango la mji, alikutana na watu waliokuwa wamebeba maiti wakitoka nje ya mji. Huyu aliyekufa alikuwa mwana pekee wa mwanamke mjane. Umati mkubwa wa watu wa mji ule walikuwa pamoja na huyo mwanamke.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

12 Alipokaribia lango la mji, alikutana na watu waliokuwa wamebeba maiti wakitoka nje ya mji. Huyu aliyekufa alikuwa mwana pekee wa mwanamke mjane. Umati mkubwa wa watu wa mji ule ulikuwa pamoja na huyo mwanamke.

Tazama sura Nakili




Luka 7:12
20 Marejeleo ya Msalaba  

Ikawa khalafu yake, akaenda mji uitwao Nain, wanafunzi wake na watu wengi wakafuatana nae.


Na Bwana alipomwona, akamhurumia, akamwambia, Usilie.


kwa sababu ana binti, mwana wa pekee, umri wake amepata miaka thenashara, nae yu katika kufa. Na katika kwenda kwake makutano wakamsonga.


Akasema, Msilie; kwa maana hakufa, bali amelala usingizi.


na watu wengi katika Wayahudi wamekuja kwa Martha na Mariamu, illi kuwafariji kwa ajili ya ndugu yao.


Petro akaondoka akafuatana nao. Alipofika wakampeleka juu orofani: wajane wote wakasimama karibu nae, wakilia na kuniwonyesha zile kanzu na nguo alizozifanya Paa wakati ule alipokuwa pamoja nao.


Akampa mkono, akamwinua; hatta akiisha kuwaita wale watakatifu na wajane akamweka mbele yao, yu hayi.


Dini iliyo safi na isiyo na taka mbele za Mungu Baba ni hii, Kwenda kuwatazama yatima na wajane katika shidda yao, na kujilinda pasipo mawaa katika dunia.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo