Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Luka 6:47 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

47 Killa mtu ajae kwangu na kuyasikia maneno yangu na kuyatenda nitawaonyesha mfano wake mtu huyu.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

47 Nitawapeni mfano unaofaa kuonesha alivyo yeyote yule anayekuja kwangu, akasikia maneno yangu na kuyatimiza:

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

47 Nitawapeni mfano unaofaa kuonesha alivyo yeyote yule anayekuja kwangu, akasikia maneno yangu na kuyatimiza:

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

47 Nitawapeni mfano unaofaa kuonesha alivyo yeyote yule anayekuja kwangu, akasikia maneno yangu na kuyatimiza:

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

47 Nitawaonesha jinsi alivyo mtu yule anayekuja kwangu na kusikia maneno yangu na kuyatenda.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

47 Nitawaonyesha jinsi alivyo mtu yule anayekuja kwangu na kusikia maneno yangu na kuyatenda.

Tazama sura Nakili




Luka 6:47
30 Marejeleo ya Msalaba  

Kwa maana ye yote atakaeyafanya mapenzi ya baba yangu aliye mbinguni, huyu ndiye ndugu yangu, na umbu langu, na mama yangu.


Alipokuwa akisema, wingu jeupe likawatia uvuli; sauti ikatoka katika lile wingu, ikinena, Huyu ni Mwanangu, mpendwa wangu, niliyependezwa nae; msikieni yeye.


Lakini yeye akasema, Bali afadhali wa kheri wenye kulisikia neno la Mungu na kulishika.


Mtu akija kwangu, nae hamehukii baba yake, na mama yake, na mke wake, na wanawe, na ndugu zake wanaume na wanawake, na uzima wake pia, hawezi kuwa mwanafunzi wangu.


Mfano wake ni mtu ajengae nyumba, akafukua, akachimba chini sana, akaweka msingi wake juu ya mwamba. Bassi palipokuwa na gharika, mto ukairukia nyumba ile kwa nguvu, usiweze kuitikisa, kwa kuwa msingi wake umewekwa juu ya mwamba.


Na wale juu ya mwamba ndio wale ambao, walisikiapo neno, hulipokea kwa furaha; na hawa hawana mizizi, huamini kwa kitambo, na wakati wa kujaribiwa hujitenga.


Nyingine zikaanguka penye udongo mwema, zikamea, zikazaa mia mia. Alipokuwa akinena haya, akapaaza sauti yake, akisema, Mwenye masikio ya kusikilia, na asikie.


Kondoo zangu waisikia sauti yangu, nami nawajua, nao wanifuata;


Mkiyajua hayo, m kheri mkiyatenda.


Mkinipenda mtazishika amri zangu.


wala hamtaki kuja kwangu, mpate kuwa na uzima.


Yesu akawaambia, Mimi ni mkate wa uzima; yeye ajae kwangu hataona njaa kabisa, nae aniaminiye hataona kiu kamwe.


Yote anipayo Bwana itakuja kwangu; nae ajae kwangu sitamtupa nje kamwe.


Bassi Wayahudi wakamwambia, Sasa tumefahamu ya kuwa una pepo; Ibrahimu amekufa na manabii, na wewe wasema, Mtu akilishika neno langu, hataonja mauti kabisa hatta milele.


nae alipokwisha kukamilishwa, akawa sababu ya wokofu wa milele kwa watu wote wanaomtii;


Bassi yeye ajuae kutenda mema, wala hayatendi, kwake huyu ni dhambi.


Mkimwendea yeye, jiwe lililo hayi, lililokataliwa na wana Adamu, bali kwa Mungu ni teule, lenye thamani,


Kwa hivo ndugu, jitahidini zaidi kufanya imara wito wenu na uteule wenu; maana mkitenda hayo hamtajikwaa kamwe.


Kama mkijua ya kuwa yeye ni mwenye haki, jueni ya kuwa killa atendae haki amezaliwa nae.


Wanangu, mtu asikudanganyeni; afanyae haki yuna haki, kama yeye alivyo na haki;


Wa kheri wazifuazo nguo zao, wawe na amri kuuendea mti wa uzima, na kuuingia mji kwa milango yake.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo