Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Luka 6:45 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

45 Mtu mwema katika hazina njema ya moyo wake hutoa lililo jema: na mtu mwovu katika hazina mbovu ya moyo wake hutoa lililo ovu: kwa sababu kinywa cha mtu huyanena yaujazayo moyo wake.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

45 Mtu mwema hutoa yaliyo mema kutoka katika hazina bora iliyomo moyoni mwake; na mtu mbaya hutoa yaliyo mabaya kutoka katika hazina mbaya iliyo moyoni mwake, kwa maana mtu huongea kutokana na yale yaliyojaa moyoni mwake.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

45 Mtu mwema hutoa yaliyo mema kutoka katika hazina bora iliyomo moyoni mwake; na mtu mbaya hutoa yaliyo mabaya kutoka katika hazina mbaya iliyo moyoni mwake, kwa maana mtu huongea kutokana na yale yaliyojaa moyoni mwake.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

45 Mtu mwema hutoa yaliyo mema kutoka katika hazina bora iliyomo moyoni mwake; na mtu mbaya hutoa yaliyo mabaya kutoka katika hazina mbaya iliyo moyoni mwake, kwa maana mtu huongea kutokana na yale yaliyojaa moyoni mwake.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

45 Vivyo hivyo mtu mwema hutoa mambo mema kutoka hazina ya moyo wake, naye mtu mwovu hutoa mambo maovu kutoka hazina ya moyo wake. Kwa kuwa mtu hunena kwa kinywa chake yale yaliyoujaza moyo wake.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

45 Vivyo hivyo mtu mwema hutoa mambo mema kutoka kwenye hazina ya moyo wake, naye mtu mwovu hutoa mambo maovu kutoka kwenye hazina ya moyo wake. Kwa kuwa mtu hunena kwa kinywa chake yale yaliyoujaza moyo wake.

Tazama sura Nakili




Luka 6:45
31 Marejeleo ya Msalaba  

Aniaminiye mimi, kama maandiko yalivyonena, mito ya maji ya uzima itamtoka tumhoni.


Petro akamwambia, Anania, kwa nini Shetani amekujaza moyo kumwambia uwongo Roho Mtakatifu, na kuzuia kwa siri sehemu ya thamani ya uwanja?


Mimi, niliye mdogo kuliko yeye aliye mdogo wa watakatifu wote, nilipewa neema hii, kuwakhubiri Mataifa utajiri wake Kristo usiopimika;


Neno lo lote lililo ovu lisitoke vinywani mwenu, bali lililo jema la kumfaa mwenye kuhitaji, liwape neema wanaosikia.


mkisemezana kwa zaburi na fenzi na nyimbo za roho, mkiimba na kumshangilia Bwana mioyoni mwenu;


Neno la Kristo likae kwa wingi ndani yenu katika hekima yote, mkifundishana na kuonyana kwa zaburi, na nyimbo, na tenzi za rohoni; kwa neema mkimwimbia Bwana mioyoni mwenu.


Maneno yenu yawe na neema siku zote, yakikolea chumvi, mpate kujua jinsi iwapasa vyo kumjibu killa mtu.


Maana hili ndilo agano nitakalofanyana na nyumba ya Israeli baada ya siku zile, asema Bwana; nitatia sharia zangu katika nia zao, na katika mioyo yao nitaziandika; nami mtakuwa Mungu kwao, nao watakuwa watu waugu.


illi afanye hukumu juu ya waiu wote, na kuwaadhibisha wote wasiomcha Mungu, kwa ajili ya kazi zao zote walizoziteuda bila kumcha Mungu, na kwa ajili ya maneno magumu yote ambayo hawo wenye dhambi wasiomcha Mungu wameyanena juu yake.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo