Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -

Luka 6:42 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

42 Au wawezaje kumwambia ndugu yako, Ndugu, niache niondoe kibanzi kilichomo jichoni mwako, na wewe mwenyewe huioni boriti iliyomo jichoni mwako? Mnafiki, toa kwanza boriti iliyomo jichoni mwako, ndipo utakapoona vema kutoa kibanzi jichoni mwa ndugu yako.

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

42 Au, wawezaje kumwambia ndugu yako, ‘Ndugu, ngoja nikuondoe kibanzi jichoni mwako,’ na huku huioni boriti iliyomo katika jicho lako mwenyewe? Mnafiki wewe! Toa kwanza boriti iliyomko jichoni mwako, na hapo ndipo utaona sawasawa kiasi cha kuweza kuondoa kibanzi kilicho jichoni mwa ndugu yako.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

42 Au, wawezaje kumwambia ndugu yako, ‘Ndugu, ngoja nikuondoe kibanzi jichoni mwako,’ na huku huioni boriti iliyomo katika jicho lako mwenyewe? Mnafiki wewe! Toa kwanza boriti iliyomko jichoni mwako, na hapo ndipo utaona sawasawa kiasi cha kuweza kuondoa kibanzi kilicho jichoni mwa ndugu yako.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

42 Utawezaje kumwambia ndugu yako, ‘Ndugu yangu, acha nitoe kibanzi kilicho ndani ya jicho lako,’ wakati wewe mwenyewe huoni boriti iliyo ndani ya jicho lako? Ewe mnafiki, ondoa boriti ndani ya jicho lako kwanza, ndipo utaweza kuona dhahiri jinsi ya kuondoa kibanzi kilicho ndani ya jicho la ndugu yako.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

Luka 6:42
24 Marejeleo ya Msalaba  

Petro akalikumbuka lile neno la Yesu aliloambiwa nae, Kabla ya kuwika jogoo, utanikana marra tatu. Akatoka nje, akalia kwa majonzi.

Nawe, ya nini kukitazama kibanzi kilicho katika jicho la ndugu yako, na boriti iliyo katika jicho lako huiangalii?

Au utamwambiaje ndugu yako, Niache niondoe kibanzi katika jicho lako; na kumbe! imo boriti ndani ya jicho lako?

Bassi Bwana akamjibu, akasema, Ewe mnafiki, killa mmoja wenu je! hamfungui ngʼombe wake au punda wake mazizini siku ya sabato, akaenda nae kumnywesha?

lakini nimekuombea, illi imani yako isipunguke; nawe uongokapo, wathubutishe ndugu zako.

Bassi, mbona watazama kibanzi kilichomo jichoni mwa ndugu yako, na boriti iliyomo jichoni mwako huioni?

Maana hapana mti mwema uzaao matunda mabovu; wala mti mbovu uzaao matunda mema.

Ewe mwenye kujaa hila na uovu wote, mwana wa shetani, adui wa haki yote, huachi kuzipotoa njia za Bwana zilizonyoka?

Petro akawaambia, Tubuni mkabatizwe killa mmoja kwa jina lake Yesu Kristo, mpate ondoleo la dhambi, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu.

Huna fungu wala huna sehemu katika jambo hili, kwa kuwa moyo wako si mnyofu mbele ya Mungu.

KWA hiyo, ee mtu uhukumuye uwae yote, huna udhuru; kwa maana katika hayo uhukumuyo mwingine wajihukumu nafsi yako; kwa maana wewe uhukumuye unafanya yale yale.

Lakini vyote pia vyatokana na Mungu, aliyetupatanisha sisi na nafsi yake kwa Kristo, nae alitupa khuduma ya upatauisho;

Bassi ikiwa mtu amejitakasa kwa kujitenga na hawa atakuwa chombo cha kupata heshima, kilichosafishwa, kimfaacho Bwana, kimetengenezwa kwa killa kazi iliyo njema.

Maana yeye asiyekuwa na haya ni kipofu, hawezi kuona vitu vilivyo mbali, amesahau kule kutakaswa dhambi zake za zamani.

Tufuate:

Matangazo

Matangazo