Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Luka 6:30 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

30 Killa akuombae mpe; nae akunyangʼanyae mali zako, usitake akurudishie.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

30 Yeyote anayekuomba mpe, na mtu akikunyanganya mali yako usimtake akurudishie.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

30 Yeyote anayekuomba mpe, na mtu akikunyanganya mali yako usimtake akurudishie.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

30 Yeyote anayekuomba mpe, na mtu akikunyang'anya mali yako usimtake akurudishie.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

30 Mpe kila akuombaye, na kama mtu akichukua mali yako usitake akurudishie.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

30 Mpe kila akuombaye, na kama mtu akichukua mali yako usitake akurudishie.

Tazama sura Nakili




Luka 6:30
29 Marejeleo ya Msalaba  

Vivyo hivyo na Baba yangu wa mbinguni atawatenda ninyi, kama ninyi kwa mioyo yenu hamkusamehe killa mtu ndugu yake makosa yake.


bali mimi nawaambieni, Msishindane na mtu mwovu; bali mtu akupigae shavu la kuume, mgeuzie na la pili.


Utusamehe deni zetu, kama sisi tunavyowasamehe wadeni wetu.


Lakini toeni sadaka vile vya ndani, na tazama, vitu vyote ni safi kwemi.


Viuzeni mlivyo navyo, katoeni sadaka, jifanyieni mifuko isiyochakaa, akiba isiyopungua katika mbingu, asikokaribia mwizi, wala nondo kuharibu.


Yesu aliposikia haya, akamwambia, Neno moja hujalipata bado; viuze vitu vyote ulivyo navyo, ukawagawie maskini, nawe utakuwa na hazina mbinguni. Kiisha, njoo unifuate.


Akupigae shavu moja, umgeuzie la pili, nae akunyangʼanyae joho yako usimzuilie na kanzu.


Na kama mnavyotaka watu wawatendee ninyi, nanyi watendeeni vivyo hivyo.


Toeni, nanyi mtapewa: kipimo chema kilichoshindiliwa, kilichosukwasukwa, kinachofurika ndicho watu watakachowapa ninyi kifuani mwenu. Kwa maana kipimo kile kile mpimacho, ndicho mtakachopimiwa na ninyi.


Nimewapeni mfano katika mambo yote ya kuwa kwa kushika kazi hivi imewapaseni kuwasaidia wasio na nguvu, na kuyakumbuka maneno ya Bwana Yesu, jinsi alivyosema mwenyewe, Ni kheri kutoa kuliko kupokea.


Maana mmejua neema ya Bwana wetu Yesu Kristo, jinsi alivyokuwa maskini kwa ajili yetu, alipokuwa tajiri, illi ninyi mpate kuwa matajiri kwa umaskini wake.


Mwibaji asiibe tena; bali afadhali afanye juhudi, akitenda kazi iliyo njema kwa mikono yake mwenyewe, apafe kuwa na kitu cha kumgawia mhitaji.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo