Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Luka 6:28 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

28 wabarikini wao wawalaanio ninyi, waombeeni wao watendao ninyi jeuri.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

28 Watakieni baraka wale wanaowalaani, na waombeeni wale wanaowatendea vibaya.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

28 Watakieni baraka wale wanaowalaani, na waombeeni wale wanaowatendea vibaya.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

28 Watakieni baraka wale wanaowalaani, na waombeeni wale wanaowatendea vibaya.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

28 Wabarikini wale wanaowalaani, waombeeni wale wanaowatendea mabaya.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

28 Wabarikini wale wanaowalaani, waombeeni wale wanaowatendea mabaya.

Tazama sura Nakili




Luka 6:28
13 Marejeleo ya Msalaba  

bali mimi nawaambieni, Wapendeni adui zenu, wabarikini wanaowalaani, watendeni mema wanaowachukia, waombeeni wanaowatendea ukorofi, na kuwatesa;


Yesu akasema, Baba, uwasamehe, kwa maana hawajui watendalo. Wakagawanya nguo zake, wakipiga kura.


Bali nawaambia ninyi mnaosikiliza, Wapendeni adui zenu, watendeni mema wao wawachukiao ninyi,


Bali wapendeni adui zenu, katendeni kwa ihsani, kopeshani, bali kutumaini kupata kitu tena: na thawabu yenu itakuwa nyingi, na mtakuwa wana wa Aliye juu sana; kwa sabahu Yeye yu mwema kwa watu wasio na shukrani, na waovu.


Hatta palipotokea shambulio la watu wa mataifa na Wayahudi pamoja na wakubwa wao juu yao, kuwatenda jeuri na kuwapiga mawe,


Akapiga magoti, akalia kwa sauti kuu, Bwana, usiwahesabie dhambi hii. Akiisha kusema haya akalala.


Wabarikini wanaowafukuzeni; barikini, wala msilaani.


tena twataabika tukifanya kazi kwa mikono yetu wenyewe. Tukitukanwa twabariki, tukiudhiwa twavumilia;


Katika kinywa kile kile hutoka baraka na laana. Ndugu zangu, mambo haya hayapasi kuwa hivyo.


watu wasiolipa baya badala ya baya, au laumu badala ya laumu; bali wabarikio; kwa sababu ndiyo mlioitiwa illi mrithi baraka.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo