Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Luka 6:22 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

22 M kheri ninyi, wana Adamu watakapowachukieni na watakapowaharamisha, na kuwashutumu, na kulitupa nje jina lenu kuma kitu kiovu, kwa ajili yake Mwana wa Adamu.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

22 “Heri yenu nyinyi iwapo watu watawachukia, watawatenga, watawatukana na kuwaharibieni jina kwa ajili ya Mwana wa Mtu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

22 “Heri yenu nyinyi iwapo watu watawachukia, watawatenga, watawatukana na kuwaharibieni jina kwa ajili ya Mwana wa Mtu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

22 “Heri yenu nyinyi iwapo watu watawachukia, watawatenga, watawatukana na kuwaharibieni jina kwa ajili ya Mwana wa Mtu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

22 Mmebarikiwa ninyi, watu watakapowachukia, watakapowatenga na kuwatukana na kulikataa jina lenu kama neno ovu, kwa ajili ya Mwana wa Adamu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

22 Mmebarikiwa ninyi, watu watakapowachukia, watakapowatenga na kuwatukana na kulikataa jina lenu kama neno ovu, kwa ajili ya Mwana wa Adamu.

Tazama sura Nakili




Luka 6:22
29 Marejeleo ya Msalaba  

nanyi mtachukuliwa mbele ya maliwali na wafalme kwa ajili yangu, illi kuwa ushuhuda kwao na kwa mataifa.


Na mtakuwa mkichukiwa na watu wole kwa ajili ya jina langu: lakini adumuye hatta mwisho, ndiye atakaeokoka.


Anaeipata roho yake ataiangamiza; nae anaeitoa roho yake kwa ajili yangu ataipata.


Wakamtupa nje ya shamba la mizabibu wakamwua. Bassi yule bwana wa shamba la mizabibu atawatendani?


Mtachukizwa na watu wote kwa ajili ya jina langu.


M kheri ninyi mnaoona njaa sasa: kwa subabu mtashiba. M kheri ninyi mliao sasa: kwa sababu mtacheka.


Walakini hatta katika wakubwa wengi walimwamini; lakini kwa sababu ya Mafarisayo hawakumwungama, wasije wakalolewa katika masunagogi.


Watawaharamisha masunagogi: naam, saa inakuja, atakapodhani killa mtu awauae kuwa amtolea Mungu ibada.


Mimi nimewapa neno lako; na ulimwengu uliwachukia, kwa kuwa wao si watu wa ulimwengu, kama mimi nisivyo wa ulimwengu.


Ulimwengu hauwezi kuwachukia ninyi: bali hunichukia mimi, kwa sababu mimi naushuhudia ya kuwa kazi zake ni mbovu.


Wakajibu, wakamwambia, Wewe ulizaliwa katika dhambi tupu, nawe unatufuudisha sisi? Wakamtoa nje.


Wakamsikiliza mpaka neno lile, wakapaaza sauti zao, wakisema, Mwondoe huyu katika inchi, kwa maana haifai aishi.


Kwa maana tamemwona mtu huyu mkorofi, muanzishaji wa fitina katika Mayahudi waliomo duniani, tena ni kichwa cha uzushi wa Wanazorayo.


Maana nitamwonyesba mambo mengi makuu yatakayompasa kuteswa kwa ajili ya Jina langu.


Yu kheri astahimiliye majaribu; kwa sababu akipata kibali ataipokea taji ya uzima, Bwana aliyowaahidia wampendao.


Lakini mjapoteswa kwa sababu ya haki, in kheri; msiogope kutisha kwao, wala msifadhaike;


Tufuate:

Matangazo


Matangazo