Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -

Luka 6:17 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

17 Akatelemka pamoja nao, akasimama panapo uwanda, pamoja na kundi la wanafunzi wake, na kundi la watu waliotoka Yahudi wote, na Yerusalemi, na pwani ya Turo na Sidon, waliokuja wamsikilize na kuponywa maradhi zao;

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

17 Baada ya kushuka mlimani pamoja nao, Yesu alisimama mahali palipokuwa tambarare. Hapo kulikuwa na kundi kubwa la wanafunzi wake na umati wa watu waliotoka pande zote za Yudea na Yerusalemu na pwani ya Tiro na Sidoni. Wote walifika kumsikiliza Yesu na kuponywa magonjwa yao.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

17 Baada ya kushuka mlimani pamoja nao, Yesu alisimama mahali palipokuwa tambarare. Hapo kulikuwa na kundi kubwa la wanafunzi wake na umati wa watu waliotoka pande zote za Yudea na Yerusalemu na pwani ya Tiro na Sidoni. Wote walifika kumsikiliza Yesu na kuponywa magonjwa yao.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

17 Akashuka pamoja nao, akasimama mahali penye uwanja tambarare. Hapo palikuwa na idadi kubwa ya wanafunzi wake na umati mkubwa wa watu kutoka sehemu zote za Yudea, kutoka Yerusalemu, na kutoka pwani ya Tiro na Sidoni.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

17 Akashuka pamoja nao, akasimama mahali penye uwanja tambarare. Hapo palikuwa na idadi kubwa ya wanafunzi wake na umati mkubwa wa watu kutoka sehemu zote za Uyahudi, kutoka Yerusalemu, na kutoka pwani ya Tiro na Sidoni.

Tazama sura Nakili

Luka 6:17
14 Marejeleo ya Msalaba  

Ole wako, Korazin! Ole wako, Bethsaida! Kwa maana kama miujiza iliyofanyika kwenu ingalifanyika katika Turo na Sidon, wangalitubu zamani kwa kuvaa gunia na majivu.

Nae Yesu akijua haya akatoka huko: makutano mengi wakamfuata; akawaponya wote,

Yesu akatoka, akaona makutano mengi, akawahurumia, akawaponya wagonjwa wao.

Yesu akatoka huko, akaenda pande za Turo na Sidon.

NAE akivaona makutano, akapanda mlimani; na alipokwisha kuketi, wanafunzi wake wakamjia;

Lakini khabari zake zikazidi kuenea, wakakutana makutano mengi kumsikiliza na kuponywa magonjwa yao.

Ikawa katika siku zile akaomloka akaenda mlimani kuomba, akashinda usiku kucha, akimwomba Mungu.

Yuda wa Yakobo; na Yuda Iskariote, ndiye aliyekuwa khaini.

nao waliosumbuliwa na pepo wachafu; wakaponywa.

Tufuate:

Matangazo

Matangazo