Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Luka 5:30 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

30 Mafarisayo na waandishi wao wakawanungʼunikia wanafunzi wake, wakisema, Kwa nini mnakula na kunywa pamoja na watoza ushuru na wenye dhambi?

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

30 Mafarisayo na waalimu wa sheria wakawanungunikia wanafunzi wake wakisema: “Kwa nini mnakula na kunywa pamoja na watozaushuru na wenye dhambi?”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

30 Mafarisayo na waalimu wa sheria wakawanungunikia wanafunzi wake wakisema: “Kwa nini mnakula na kunywa pamoja na watozaushuru na wenye dhambi?”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

30 Mafarisayo na waalimu wa sheria wakawanung'unikia wanafunzi wake wakisema: “Kwa nini mnakula na kunywa pamoja na watozaushuru na wenye dhambi?”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

30 Lakini Mafarisayo na walimu wa Torati waliokuwa wa dhehebu lao wakawalalamikia wanafunzi wa Isa, wakisema, “Mbona mnakula na kunywa pamoja na watoza ushuru na wenye dhambi?”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

30 Lakini Mafarisayo na walimu wa Torati waliokuwa wa dhehebu lao wakawalalamikia wanafunzi wa Isa, wakisema, “Mbona mnakula na kunywa pamoja na watoza ushuru na ‘wenye dhambi’?”

Tazama sura Nakili




Luka 5:30
16 Marejeleo ya Msalaba  

Maana mkiwapenda wanaowapendani, mwapata thawabu gani? Hatta watoza ushuru, je, nao hawafanyi yayo hayo?


Mafarisayo walipoona, wakawaambia wanafunzi wake, Kwa nini mwalimu wenu anakula pamoja na watoza ushuru na wenye dhambi?


Na waandishi na Mafarisayo walipomwona anakula pamoja na watoza ushuru na wenye dhambi, waliwaambia wanafunzi wake, Kwa nini anakula na kunywa pamoja na watoza ushuru na wenye dhambi?


Kwa maana Mafarisayo na Wayahudi wote wasiponawa mikono kwanza, hawali, wakishika hadithi za wazee wao:


Akawauliza wale waandishi, Nini mnajadiliana nao?


Yule Farisayo akasimama, akasali hivi kwa nafsi yake, Mungu, nakushukuru kwa sababu mimi si kama watu wengine, wanyangʼanyi, wazinzi, waia kama na huyu mtoza ushuru.


Hatta watu walipoona wakanungʼunika wote, wakisema, ya kama, Ameingia akae kwa mtu mwenye dhambi.


Hatta siku moja ya siku zile alikuwa akifundisha, na Mafarisayo na waandishi wameketi, waliokuwa wametoka katika killa kijiji cha Galilaya, na cha Yahudi, na Yerusalemi; uweza wa Bwana ulikuwa pamoja nae apate kuwaponya.


Wale waandishi na Mafarisayo wakaanza kutafakari wakanena, Nani huyu anaesema kufuru? Nani awezae kuondoa dhambi, isipokuwa mmoja ndiye Mungu?


Mwana wa Adamu amekuja, anakula na kunywa, mkasema, Mlafi huyu, na mnywaji wa mvinyo, rafiki wa watoza ushuru na wenye dhambi.


Yule Farisayo aliyemwalika, alipoona haya akasema kimoyomoyo, akinena, Mtu huyu kama angekuwa nabii, angalimjua huyu ni nani! na ni mwanamke gani anaemgusa, ya kuwa ni mwenye dhambi.


Pakawa makelele mengi. Waandishi wa upande wa Mafarisayo wakasimama, wakamtetea, wakisema, Hatuoni uovu wo wote katika mtu huyu; bali ikiwa roho au malaika amesema nae tusishindane na Mungu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo