Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Luka 5:26 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

26 Ushangao ukawashika wote wakamtukuza Mungu: wakajaa khofu, wakinena, Tumeona maajabu leo.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

26 Wote wakashangaa na kushikwa na hofu; wakamtukuza Mungu wakisema: “Tumeona maajabu leo.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

26 Wote wakashangaa na kushikwa na hofu; wakamtukuza Mungu wakisema: “Tumeona maajabu leo.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

26 Wote wakashangaa na kushikwa na hofu; wakamtukuza Mungu wakisema: “Tumeona maajabu leo.”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

26 Kila mmoja akashangaa na kumtukuza Mungu. Wakajawa na hofu ya Mungu, wakasema, “Leo tumeona mambo ya ajabu.”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

26 Kila mmoja akashangaa na kumtukuza Mungu. Wakajawa na hofu ya Mungu, wakasema, “Leo tumeona mambo ya ajabu.”

Tazama sura Nakili




Luka 5:26
13 Marejeleo ya Msalaba  

Makutano wote wakashangaa wakasema, Huyu siye mwana wa Daud?


Wakaondoka upesi kutoka kaburini, kwa khofu na furaha nyingi, wakaenda mbio kuwapasha wanafunzi wake khabari.


Makutano wakimwona, wakastaajabu, wakamtukuza Mungu, aliyewapa watu mamlaka ya jinsi hii.


Akaondoka marra, akajitwika kitanda chake, akatoka mbele yao wote; hatta wakastaajabu wote, wakamtukuza Mungu, wakinena, Namna hii hatujapata kuyaona kamwe.


Khofu ikawaingia wote waliokaa karibu nao; yakaenea maneno haya pia milimani mwote Uyahudi.


Simon Petro alipoona haya, akaanguka magotini pa Yesu, akasema, Toka kwangu, kwa sababu mimi ni mtu mwenye dhambi, Bwana.


Khofu ikawashika wote, wakamtukuza Mungu, wakisema, Nabii mkuu ametokea kwetu: na Mungu amewajilia watu wake.


Na watu wote wa inchi ya Wagadarene iliyo kando kando wakamwomba aondoke kwao, kwa sababu walishikwa na khofu nyingi; bassi akakiingia chombo akarudi.


Nao walipokwisha kuwaogofya tena wakawafungua, wasione njia ya kuwaadhibu, kwa sababu ya watu: kwa kuwa watu wote walikuwa wakimtukuza Mungu kwa hayo yaliyotendeka:


Wakamtukuza Mungu kwa ajili yangu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo