Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Luka 5:24 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

24 Lakini mpate kujua ya kuwa Mwana wa Adamu ana mamlaka duniani ya kuondoa dhambi (alimwambia yule mwenye kupooza), Nakuambia, Ondoka, ujitwike kitanda chako ukaende nyumbani kwako.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

24 Basi, nataka mjue kwamba Mwana wa Mtu anao uwezo wa kuwasamehe watu dhambi duniani.” Hapo akamwambia huyo mtu aliyepooza, “Simama, chukua kitanda chako, uende zako nyumbani.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

24 Basi, nataka mjue kwamba Mwana wa Mtu anao uwezo wa kuwasamehe watu dhambi duniani.” Hapo akamwambia huyo mtu aliyepooza, “Simama, chukua kitanda chako, uende zako nyumbani.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

24 Basi, nataka mjue kwamba Mwana wa Mtu anao uwezo wa kuwasamehe watu dhambi duniani.” Hapo akamwambia huyo mtu aliyepooza, “Simama, chukua kitanda chako, uende zako nyumbani.”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

24 Lakini ili mpate kujua kwamba Mwana wa Adamu anayo mamlaka duniani kusamehe dhambi.” Akamwambia yule aliyepooza, “Nakuambia, inuka, chukua mkeka wako, uende nyumbani mwako.”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

24 Lakini ili mpate kujua kwamba Mwana wa Adamu anayo mamlaka duniani kusamehe dhambi…” Akamwambia yule aliyepooza, “Nakuambia, inuka, chukua mkeka wako, uende nyumbani kwako.”

Tazama sura Nakili




Luka 5:24
26 Marejeleo ya Msalaba  

Yesu akaenda pande za Kaisaria Filipi, akawauliza wanafunzi wake akinena, Watu huninena mimi, Mwana wa Adamu, kuwa nani?


Hatta atakapokuja Mwana wa Adamu katika utukufu wake, na malaika watakatifu wote pamoja nae, ndipo atakapoketi katika kiti cha utukufu wake:


Yesu akamwambia. Wewe umesema: lakini nawaambieni, Tangu sasa mtamwoua Mwana wa Adamu ameketi mkono wa kuume wa nguvu, akija juu ya mawingu.


Yesu akaja kwao, akasema nao, akinena, Nimepewa mamlaka yote mbinguni na juu ya dunia.


Khabari zake zikaenea katika Sham yote; wakamletea watu waliokuwa hawawezi, walioshikwa mi maradhi mbali mbali na mateso, nao wenye pepo, na wenye kifafa, na wenye kupooza; akawaponya.


Lakini illi mjue ya kuwa Mwana wa Adamu yuna mamlaka katika dunia kuondoa dhambi, (amwambia yule mgonjwa wa kupooza) Ondoka, ujitwike kitanda chako, ukaende nyumbani kwako.


Nae akauyosha mkono wake, akamgusa, akinena, Nataka; takasika. Marra ukoma wake ukamwounoka.


Na kumbe! watu wanachukua mtu kitandani mwenye kupooza: wakitaka kumpeleka ndani na kumweka mbele yake.


Vipi vyepesi, kusema, Dhambi zako zimeondolewa, au kusema, Ondoka, ukaende.


Akaenda karibu, akaligusa jeneza; wale wachukuzi wakasimama. Akasema, Kijana, nakuambia, Ondoka.


Nae akawatoa nje wote, akamshika mkono wake, akapaaza sauti yake, akisema, Kijana, ondoka.


Akiisha kusema haya, akalia kwa sauti kuu, Lazaro, toka, njoo huku.


kama vile ulivyompa mamlaka juu ya killa mwenye mwili, illi yote uliyompa awape uzima wa milele.


Na hapana mtu aliyepanda mbinguni, illa yeye aliyeshuka kutoka mbinguni, Mwana wa Adamu alioko mbinguni.


akampa mamlaka ya kufanya hukumu kwa sababu yu Mwana wa Adamu.


akanena kwa sauti kuu, Simama kwa miguu yako sawa sawa. Akasimama upesi akaenda.


Mtu kuyo Mungu amemtukuza kwa mkono wake wa kuume, awe Mkuu na Mwokozi, awape Waisraeli toha na masamaha ya dhambi.


Petro akamwambia, Ainea, Yesu Kristo akuponya: ondoka, ukatandike kitanda chako.


Petro akawatoa wote, akapiga magoti, akaomba, akaielekea mayiti, akanena, Tabitha, ondoka. Nae akafumbua macho yake, na alipomwona Petro akajiinua, akaketi.


na kati kati ya vile vinara nikaona mtu kwa mfano wa Mwana Adamu, amevaa vazi lililofika miguuni, na kufungwa mshipi wa dhahabu matitini.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo