Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Luka 5:17 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

17 Hatta siku moja ya siku zile alikuwa akifundisha, na Mafarisayo na waandishi wameketi, waliokuwa wametoka katika killa kijiji cha Galilaya, na cha Yahudi, na Yerusalemi; uweza wa Bwana ulikuwa pamoja nae apate kuwaponya.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

17 Siku moja, Yesu alikuwa akifundisha. Mafarisayo na waalimu wa sheria kutoka katika kila kijiji cha Galilaya, Yudea na Yerusalemu, walikuwa wameketi hapo. Nguvu ya Bwana ilikuwa pamoja naye kwa ajili ya kuponya wagonjwa.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

17 Siku moja, Yesu alikuwa akifundisha. Mafarisayo na waalimu wa sheria kutoka katika kila kijiji cha Galilaya, Yudea na Yerusalemu, walikuwa wameketi hapo. Nguvu ya Bwana ilikuwa pamoja naye kwa ajili ya kuponya wagonjwa.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

17 Siku moja, Yesu alikuwa akifundisha. Mafarisayo na waalimu wa sheria kutoka katika kila kijiji cha Galilaya, Yudea na Yerusalemu, walikuwa wameketi hapo. Nguvu ya Bwana ilikuwa pamoja naye kwa ajili ya kuponya wagonjwa.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

17 Siku moja Isa alipokuwa akifundisha, Mafarisayo na walimu wa Torati, waliokuwa wametoka kila kijiji cha Galilaya na kutoka Yudea na Yerusalemu, walikuwa wameketi huko. Nao uweza wa Mwenyezi Mungu ulikuwa juu yake kuponya wagonjwa.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

17 Siku moja Isa alipokuwa akifundisha, Mafarisayo na walimu wa Torati, waliokuwa wametoka kila kijiji cha Galilaya na kutoka Uyahudi na Yerusalemu, walikuwa wameketi huko. Nao uweza wa Mwenyezi Mungu ulikuwa juu yake kuponya wagonjwa.

Tazama sura Nakili




Luka 5:17
20 Marejeleo ya Msalaba  

vipofu wanapata kuona, viwete wanatembea, wenye ukoma wanatakasika, viziwi wanasikia, wafu wanafufuliwa, na maskini wanakhubiriwa khabari njema.


NDIPO waandishi na Mafarisayo toka Yerusalemi wakamwendea Yesu wakinena,


Nae akatoka, akaanza kukhubiri mengi, na kulitangaza lile neno, hatta Yesu asiweze tena kuingia mjini kwa wazi; bali alikuwa nje mabali pasipo watu; wakamwendea kutoka killa pahali.


watashika nyoka; hatta wakinywa kitu cha kufisha, hakitawadhuru kabisa; wataweka mikono yao juu ya wagonjwa, nao watapata afya.


Waandishi walioshuka kutoka Yahudi wakanena, Ana Beelzebul, na kwa uwezo wa mkuu wa pepo awafukuza pepo.


Marra Yesu akifahamu nafsini mwake kwamba nguvu zimemtoka, akageuka kati ya makutano, akanena, Ni nani aliyenigusa mavazi yangu?


KIISHA Mafarisayo na baadhi ya waandishi waliotoka Yerusalemi wakakusanyika mbele yake,


Mafarisayo na wandishi wakanungʼunika, wakasema, Huyu hukaribisha wenye dhambi, hula pamoja nao.


Ikawa baada ya siku tatu, wakamwona hekaluni, ameketi kati ya waalimu, akiwasikiliza, na kuwauliza.


Wale waandishi na Mafarisayo wakaanza kutafakari wakanena, Nani huyu anaesema kufuru? Nani awezae kuondoa dhambi, isipokuwa mmoja ndiye Mungu?


Mafarisayo na waandishi wao wakawanungʼunikia wanafunzi wake, wakisema, Kwa nini mnakula na kunywa pamoja na watoza ushuru na wenye dhambi?


Makutano yote wakatafuta kumgusa: kwa maana nguvu zilikuwa zikimtoka, zikawaponya wote.


Bali Mafarisayo na wana sharia walijikatalia shauri la Mungu kwa kuwa hawakubatizwa nae.


Yesu akasema, Mtu alinigusa, kwa kuwa naliona nguvu zimenitoka.


Yesu akajibu akamwambia, Je! Wewe u mwalimu katika Israeli, na haya huyafahamu?


hali aitendae kweli huja kwenye nuru, matendo yake yaonekane ya kuwa yametendwa katika Mungu.


Mungu akafanya kwa mikono ya Paolo miujiza ya kupita kawaida;


ukinyosha mkono wako kuponya: ishara na maajabu zifanyike kwa jina la mtumishi wako mtakatifu Yesu.


Lakini mtu mmoja, Farisayo, jina lake Gamaliel, mwalimu wa torati, mwenye kuheshimiwa na watu wote, akasimama katika baraza,


Tufuate:

Matangazo


Matangazo