Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Luka 5:1 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

1 IKAWA makutano walipomsonga, wakisikiliza neno la Mungu, yeye alikuwa akisimama kando ya ziwa la Genesareti:

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

1 Siku moja, Yesu alikuwa amesimama kando ya ziwa Genesareti, na watu wengi walikuwa wamemzunguka wakisongamana, wanasikiliza neno la Mungu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

1 Siku moja, Yesu alikuwa amesimama kando ya ziwa Genesareti, na watu wengi walikuwa wamemzunguka wakisongamana, wanasikiliza neno la Mungu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

1 Siku moja, Yesu alikuwa amesimama kando ya ziwa Genesareti, na watu wengi walikuwa wamemzunguka wakisongamana, wanasikiliza neno la Mungu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

1 Siku moja Isa alipokuwa amesimama karibu na Ziwa la Genesareti, watu wengi walimsonga ili wapate kusikia neno la Mungu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

1 Siku moja Isa alipokuwa amesimama karibu na Ziwa la Genesareti, watu wengi wakiwa wanasongana kumzunguka ili wapate kusikia neno la Mungu,

Tazama sura Nakili




Luka 5:1
21 Marejeleo ya Msalaba  

Tangu siku za Yohana Mbatizaji hatta leo ufalme wa mbinguni hupatikana kwa nguvu, nao wenye nguvu wauteka.


Na walipokwisha kuvuka, wakafika inchi ya Genesareti.


Akawaambia wanafunzi wake ya kama chombo kidogo kikae karibu nae, kwa sababu ya makutano, wasije wakamsonga.


AKAANZA kufundisha tena kando ya bahari. Wakamkusanyikia mkutano mkuliwa, hatta yeye akapanda chomboni, akakaa baharini; mkutano wote ulikuwako katika inchi kavu kando ya bahari.


Akaenda pamoja nae: makutano mengi wakamfuata, wakimsongasonga.


Hatta walipokwisha kuvuka wakafika inchi ya Genesareti, wakatia nanga.


HUKO nyuma mkutano wa watu, watu elfu nyingi walipokusanyika hatta wakakanyagana, akaanza kuwaambia wanafunzi wake khassa, Jihadharini na chachu ya Mafarisayo, yaani unafiki.


akaona vyombo viwili vimekaa kando ya ziwa: na wavuvi wametoka, wanaosha nyavu zao.


Ikawa siku mojawapo ya siku zile akapanda chomboni, yeye na wanafunzi wake, akawaambia, Na tuvuke hatta ngʼambu ya ziwa: wakatweka matanga.


Na walipokuwa wakienda kwa matanga akalala usingizi. Ikashuka dharuba ya upepo juu ya ziwa, chombo kikaanza kujaa maji, wakawa katika khatari.


Akawapa rakhusa: wale pepo wakamtoka mtu yule wakawaingia nguruwe, lile kundi likatelemka kwa kassi gengeni, wakafa baharini.


Yesu akasema, Ni nani aliyenigusa? Bassi watu wote walipokana, Petro nao walio pamoja nae wakamwambia, Bwana, Makutano wanakuzunguka na kukusonga, nawe unasema, Ni nani aliyenigusa?


Andrea, ndugu ya Simon Petro, alikuwa mmoja wa wale wawili waliomsikia Yohana na kumfuata.


BAADA ya haya Yesu alikwenda zake ngʼambu ya bahari ya Galilaya, bahari ya Tiberia.


Wakumbukeni wale waliokuwa na mamlaka juu yenu, waliowaambia neno la Mungu; tena, kwa kuuchunguza sana mwisho wa maisha zao, iigeni imani yao.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo