Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -

Luka 4:41 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

41 Pepo wakawatoka wengi wakipaaza sauti zao wakisema, Wewe u Kristo, Mwana wa Mungu. Akawakemea, asiwaache kunena, kwa sababu walijua ya kuwa yeye ndiye Kristo.

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

41 Pepo waliwatoka watu wengi, wakapiga kelele wakisema: “Wewe ni Mwana wa Mungu!” Lakini Yesu akawakemea, wala hakuwaruhusu kusema, maana walijua kwamba yeye ndiye Kristo.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

41 Pepo waliwatoka watu wengi, wakapiga kelele wakisema: “Wewe ni Mwana wa Mungu!” Lakini Yesu akawakemea, wala hakuwaruhusu kusema, maana walijua kwamba yeye ndiye Kristo.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

41 Pepo waliwatoka watu wengi, wakapiga kelele wakisema: “Wewe ni Mwana wa Mungu!” Lakini Yesu akawakemea, wala hakuwaruhusu kusema, maana walijua kwamba yeye ndiye Kristo.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

41 Pepo wachafu pia wakawatoka watu wengi, nao walipokuwa wakitoka wakapiga kelele, wakisema: “Wewe ni Mwana wa Mungu!” Lakini Isa akawakemea na kuwazuia wasiseme, kwa maana walimjua kuwa yeye ndiye Al-Masihi.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

41 Pepo wachafu pia wakawatoka watu wengi, nao walipokuwa wakitoka wakapiga kelele, wakisema: “Wewe ni Mwana wa Mungu!” Lakini Isa akawakemea na kuwazuia wasiseme, kwa maana walimjua kuwa yeye ndiye Al-Masihi.

Tazama sura Nakili

Luka 4:41
14 Marejeleo ya Msalaba  

Lakini Yesu akanyamaza. Kuhani mkuu akamjihu, akamwambia, Nakuapisha Mungu aliye hayi, utuambie kama wewe ndiwe Kristo, Mwana wa Mungu.

Mjaribu akamjia akasema, Ukiwa ndiwe Mwana wa Mungu, amuru mawe haya yawe mikate.

Ilipokuwa jioni, wakamletea wengi wenye pepo: akawafukuza pepo kwa neno lake, akawaponya wote waliokuwa hawawezi,

Wakapiga kelele, wakinena, Tuna nini nawe, Yesu, Mwana wa Mungu? Je, umekuja kutuadhibu kabla ya muhulla?

Yesu akamwambia, Angalia, usimwambie mtu; illa enenda zako, ukajionyeshe kwa kuhani, utoe sadaka kama alivyoamuru Musa, iwe ushuhuda kwao.

Yesu akamkaripia, akinena, Fumba kinywa, umtoke.

Hatta ilipokuwa jioni, na jua limekwisha kuchwa, wakamletea wote waliokuwa hawawezi, na wenye pepo.

Akaponya wengi waliokuwa na maradhi nyingine nyingine, akafukuza pepo wengi, wala hakuwaacha pepo kunena, kwa sababu walimjua.

Na pepo wachafu, killa walipomwona, wahanguka mbele yake, wakalia wakinena, Wewe ndiwe Mwana wa Mungu.

Akasimama karibu nae akaikemea ile homa, ikamwacha; marra akaondoka akawakhudumu.

lakini hizi zimeandikwa mpate kuamini kwamba Yesu ni Kristo, Mwana wa Mungu; na kwa kuamini mwe na uzima kwa jina lake.

Wewe waamini ya kuwa Mungu ni mmoja; watenda vyema. Mashetani nao waamini na kutetemeka.

Tufuate:

Matangazo

Matangazo