Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -

Luka 4:25 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

25 Lakini kwa kweli nawaambieni, Palikuwa wajane wengi katika Israeli zamani za Eliya, wakati mbingu zilipofungwa miaka mitatu na miezi sita; njaa kuu ikaingia inchi yote:

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

25 Lakini, sikilizeni! Kweli kulikuwa na wajane wengi katika nchi ya Israeli nyakati za Elia. Wakati huo mvua iliacha kunyesha kwa muda wa miaka mitatu na nusu; kukawa na njaa kubwa katika nchi yote.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

25 Lakini, sikilizeni! Kweli kulikuwa na wajane wengi katika nchi ya Israeli nyakati za Elia. Wakati huo mvua iliacha kunyesha kwa muda wa miaka mitatu na nusu; kukawa na njaa kubwa katika nchi yote.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

25 Lakini, sikilizeni! Kweli kulikuwa na wajane wengi katika nchi ya Israeli nyakati za Elia. Wakati huo mvua iliacha kunyesha kwa muda wa miaka mitatu na nusu; kukawa na njaa kubwa katika nchi yote.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

25 Lakini ukweli ni kwamba palikuwa na wajane wengi katika Israeli wakati wa Ilya, mbingu zilipofungwa kwa miaka mitatu na miezi sita pakawa na njaa kuu katika nchi nzima.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

25 Lakini ukweli ni kwamba palikuwa na wajane wengi katika Israeli wakati wa Ilya, mbingu zilipofungwa kwa miaka mitatu na miezi sita pakawa na njaa kuu katika nchi nzima.

Tazama sura Nakili

Luka 4:25
12 Marejeleo ya Msalaba  

Si halali yangu kutumia vilivyo vyangu nipendavyo? Au jicho lako ni ovn kwa sababu ya kuwa mimi mwema?

Saa ileile Yesu akashangilia katika Roho, akasema, Nakushukuru, Baba, Bwana wa mbingu na inchi, kwa kuwa umewaficha wenye hekima na busara mambo haya, ukawafunulia watoto wachanga: Naam, Baba, kwa maana ndivyo vilivyokuwa vinapendeza mbele yako.

Maana alimwambia Musa, Nitamrehemu yeye nimrehemuye, nitamhurumia yeye nimhurumiae.

La! si hivyo, ee bin-Adamu; wewe u nani umjibuye Mungu? Je! kitu kilichoumbwa kimwambie yeye aliyekiumba, Ya nini nkanifanza hivi?

ambae ndani yake sisi tumepata urithi, tukichaguliwa tangu awali kwa kusudi lake yeye afanyae yote kwa shauri la nia yake;

akiisha kutujulisha siri ya nia yake, kwa kadiri ya mapenzi yake, aliyoyakusudia katika yeye huyu,

Eliya alikuwa mwana Adamu mwenye tabia moja na sisi, akaomba kwa bidii mvua isinye: na mvua haikunya juu ya inchi muda wa miaka mitatu na miezi sita.

Hawa wana mamlaka kuzifunga mbingu, illi mvua isinye katika siku za unabii wao. Na wana mamlaka juu ya maji kuyagenza kuwa damu, na kuipiga inchi kwa killa pigo, killa watakapo.

Tufuate:

Matangazo

Matangazo