Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Luka 4:22 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

22 Wakamshuhudia wote, wakayastaajabia maneno ya neema yaliyotoka kinywani mwake: wakanena, Huyu siye Mwana wa Yusuf?

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

22 Wote wakavutiwa sana naye, wakastaajabia maneno mazuri aliyosema. Wakasema, “Je, huyu si mwana wa Yosefu?”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

22 Wote wakavutiwa sana naye, wakastaajabia maneno mazuri aliyosema. Wakasema, “Je, huyu si mwana wa Yosefu?”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

22 Wote wakavutiwa sana naye, wakastaajabia maneno mazuri aliyosema. Wakasema, “Je, huyu si mwana wa Yosefu?”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

22 Watu wote walimsifu na kuyastaajabia maneno yake yaliyojaa neema, wakaulizana, “Je, huyu si mwana wa Yusufu?”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

22 Wote waliokuwako wakamsifu na kuyastaajabia maneno yake yaliyojaa neema, wakaulizana, “Je, huyu si mwana wa Yusufu?”

Tazama sura Nakili




Luka 4:22
20 Marejeleo ya Msalaba  

Wote waliomsikia wakataajahu kwa akili zake na majibu yake.


Nao walipomwona wakashangaa sana; mama yake akamwambia, Mwanangu, kwani ukatutenda hivi? Tazama, baba yako na mimi tulikuwa tukikutafuta kwa huzuni.


Kwa maana mimi nitawapeni kinywa na hekima, ambayo watesi wenu hawataweza kuikana wala kushindana nayo.


Akaanza kuwaambia, Leo andiko hili limetimia masikioni mwenu.


Filipo akamwona Nathanaeli, akamwambia, Tumemwona yeye aliyeandikiwa na Musa katika torati, na na manabii, Yesu, mwana wa Yusuf, mtu wa Nazareti


Wakanena, Huyu siye Yesu, mwana wa Yusuf, ambae twamjua baba yake na mama yake? Bassi, anenaje huyu, Nimeshuka kutoka mbinguni?


Wale watumishi wakajibu, Hajanena kamwe mwana Adamu aliye yote kama huyu anavyonena.


lakini hawakuweza kushindana na hekima yake wala na Roho aliyosema nayo.


na maneno yenye uzima yasiyoweza kuhukumiwa, illi yule mwenye kupingana nawe ataliayarike, kwa kuwa hana neno baya la kunena juu yetu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo