Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Luka 4:20 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

20 Akakifunga chuo, akampa mkhudumu, akaketi: watu wote waliokuwa katika sunagogi wakamkazia macho.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

20 Baada ya kusoma, akafunga kile kitabu, akampa mtumishi, kisha akaketi; watu wote wakamkodolea macho.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

20 Baada ya kusoma, akafunga kile kitabu, akampa mtumishi, kisha akaketi; watu wote wakamkodolea macho.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

20 Baada ya kusoma, akafunga kile kitabu, akampa mtumishi, kisha akaketi; watu wote wakamkodolea macho.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

20 Kisha akakifunga kitabu, akamrudishia mtumishi na akaketi. Watu wote waliokuwamo katika sinagogi wakamkazia macho.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

20 Kisha akakifunga kitabu, akamrudishia mtumishi na akaketi. Watu wote waliokuwamo katika sinagogi wakamkazia macho.

Tazama sura Nakili




Luka 4:20
13 Marejeleo ya Msalaba  

Saa ile Yesu akawaambia makutano, Je, mmetoka, mfano wa watu wafukuzao mnyangʼanyi mna panga na marungu, kunitwaa? Killa siku naliketi mbele zenu hekaluni, nikifundisha, wala hamkunikamata.


akanweka katika kaburi lake jipya, alilolikata mwambani; akafingirisha jiwe kubwa hatta mlango wa kaburi, akaenda zake.


nao bawakuona la kutenda; maana watu wote waliambatana nae, wakimsikiliza.


Akapewa chuo cha nabii Isaya: bassi alipokwisha kukifunua chuo hicho, akapaona pahali palipoandikwa,


Akaanza kuwaambia, Leo andiko hili limetimia masikioni mwenu.


Akaingia chombo kimoja, kilichokuwa cha Simon, akamtaka asogeze kidogo kutoka pwani. Akakaa, akawafundisha makutano katika chombo.


Hatta assubuhi ilipokucha akaingia tena hekaluni, watu wote wakamwendea: nae akaketi akawa akiwafundisha.


Hatta siku ya sabato tukatoka nje ya lango, tukaenda kando ya mto, tukidhani ya kuwa hapo pana mahali pii kuomba; tukaketi, tukasema na wanawake waliokutana pale.


Hatta Petro alipoona haya akawajibu watu, Enyi Waisraeli, mbona mnastaajabia haya, au mbona mnatukazia macho sisi, kana kwamba tumemfanya huyu aende kwa nguvu zetu sisi, au kwa utawa wetu sisi?


Tufuate:

Matangazo


Matangazo