Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Luka 4:18 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

18 Roho ya Bwana ni juu yangu, Kwa sababu amenitia mafuia kuwakhubiri maskini khabari njema. Amenituma kuwaponya waliopondeka moyo, Kuwatangazia wafungwa kufunguliwa, na vipofu kupata kuona tena, Kuwaacha wa huru waliosetwa,

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

18 “Roho wa Bwana yu juu yangu, kwani ameniweka wakfu niwaletee maskini Habari Njema. Amenituma niwatangazie mateka uhuru wao, na vipofu watapata kuona tena; amenituma niwakomboe wanaoonewa,

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

18 “Roho wa Bwana yu juu yangu, kwani ameniweka wakfu niwaletee maskini Habari Njema. Amenituma niwatangazie mateka uhuru wao, na vipofu watapata kuona tena; amenituma niwakomboe wanaoonewa,

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

18 “Roho wa Bwana yu juu yangu, kwani ameniweka wakfu niwaletee maskini Habari Njema. Amenituma niwatangazie mateka uhuru wao, na vipofu watapata kuona tena; amenituma niwakomboe wanaoonewa,

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

18 “Roho wa Bwana Mungu Mwenyezi yu juu yangu, kwa sababu amenipaka mafuta kuwahubiria maskini Habari Njema. Amenituma kuwatangazia wafungwa kufunguliwa kwao, na vipofu kupata kuona tena, kuwaweka huru wanaoteswa,

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

18 “Roho wa Mwenyezi Mungu yu juu yangu, kwa sababu amenitia mafuta kuwahubiria maskini habari njema. Amenituma kuwatangazia wafungwa kufunguliwa kwao, na vipofu kupata kuona tena, kuwaweka huru wanaoonewa,

Tazama sura Nakili




Luka 4:18
56 Marejeleo ya Msalaba  

vipofu wanapata kuona, viwete wanatembea, wenye ukoma wanatakasika, viziwi wanasikia, wafu wanafufuliwa, na maskini wanakhubiriwa khabari njema.


Tazama, mtumishi wangu niiliyemteua; Mpendwa wangu, ambae moyo wangu umependezwa nae; Nitamtia roho yangu, Nae atuwatangazia Mataifa hukumu.


Mwanzi uliopondeka hatauvunja, Wala kitani kitokacho moshi hatakizima, Hatta aletapo hukumu yake ikashinda.


Watu waliokaa gizani Waliona mwanga mkuu, Nao waliokaa katika inchi na kivuli cha mauti, Mwanga umewazukia.


Wa kheri walio maskini wa roho; maana ufalme wa mbinguni ni wao.


Akapewa chuo cha nabii Isaya: bassi alipokwisha kukifunua chuo hicho, akapaona pahali palipoandikwa,


Nae akainua macho yake akawatazama wanafunzi wake, akasema, M kheri ninyi mlio maskini: kwa sababu ufalme wa Mungu ni wemi.


Akajibu, akawaambia, Enendeni, mkamweleze Yohana mliyoyaona na kuyasikia: vipofu wanapata kuona, viwete wanatembea, wenye ukoma wanatakasika, viziwi wanasikia, wafu wanafufuliwa, maskini wanakhubiriwa khahari njema:


Huyu akamwona kwanza Simon, ndugu yake mwenyewe, akamwambia, Tumemwona Masihi, (tafsiri yake Kristo).


Mimi nimekuja niwe nuru ulimwenguni, illi kilia aniaminiye mimi asikae gizani.


Kwa kuwa yeye aliyetumwa na Mungu huyanena maneno ya Mungu: kwa sababu Mungu hampi Roho kwa kupima.


khabari za Yesu wa Nazareti, jinsi Mungu alivyomtia mafuta kwa Roho Mtakatifu na uguvu: nae akatembea huko na huko, akitenda kazi njema na kuponya wote walioonewa na Shetani; kwa maana Mungu alikuwa pamoja nae.


uwafumhue macho yao, waiache giza na kuielekea nuru, na waziache nguvu za Shetani na kumwelekea Mungu, na wapate masamaha ya dhambi zao, na urithi miongoni mwao waliotakaswa kwa imani iliyo kwangu.


Wafalme wa dunia wamejipanga, Na wakuu wamefanya shauri pamoja, Juu ya Bwana na juu ya Kristo wake.


Maana ni kweli, Herode na Pontio Pilato pamoja na mataifa na watu wa Israeli, walikusanyika juu ya mtumishi wako mtakatifu Yesu, uliyemtia mafuta,


aliyetuokoa na uguvu za giza, akatuhamisha na kutuingiza katika ufalme wa Mwana wa pendo lake;


Sikihzeni, ndugu niwapendao, Mungu hakuwachagua maskini wa dunia wawe matajiri wa imani na warithi wa ufalme aliowaahidia wampendao?


Bali ninyi m mzao mteule, ukubani wa kifaume, taifa takatifu, watu wa milki, mpate kutangaza fadhili zake aliyewaita mtoke gizani mkaingie katika nuru yake ya ajabu;


Tufuate:

Matangazo


Matangazo