Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Luka 3:7 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

7 Bassi akawaambia makutano waliotokea illi kubatizwa nae, Enyi uzao wa nyoka, ni nani aliyewaonya kuikimbia ghadhabu itakayokuja?

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

7 Basi, Yohane akawa anawaambia watu wengi waliofika ili awabatize: “Enyi kizazi cha nyoka! Ni nani aliyewadokezea muikimbie ghadhabu inayokuja?

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

7 Basi, Yohane akawa anawaambia watu wengi waliofika ili awabatize: “Enyi kizazi cha nyoka! Ni nani aliyewadokezea muikimbie ghadhabu inayokuja?

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

7 Basi, Yohane akawa anawaambia watu wengi waliofika ili awabatize: “Enyi kizazi cha nyoka! Ni nani aliyewadokezea muikimbie ghadhabu inayokuja?

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

7 Yahya akaambia umati ule wa watu waliokuwa wanakuja ili kubatizwa naye, “Ninyi watoto wa nyoka! Ni nani aliyewaonya kuikimbia ghadhabu inayokuja?

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

7 Yahya akauambia ule umati wa watu uliokuwa unakuja ili kubatizwa naye, “Ninyi watoto wa nyoka! Ni nani aliyewaonya kuikimbia ghadhabu inayokuja?

Tazama sura Nakili




Luka 3:7
12 Marejeleo ya Msalaba  

Uzao wa nyoka, mwawezaje kusema mema, mkiwa wabaya? Maana, kinywa cha mtu huyanena yaujazayo moyo wake.


Enyi nyoka, mazao wa majoka, mtaikimbiaje hukumu ya jehannum?


wakabatizwa nae mtoni Yordani, wakiziungama dhambi zao.


Ninyi wa baba yenu Shetani, na tamaa za baba yenu ndizo mpendazo kuzifanya. Yeye alikuwa mwuaji tangu mwanzo, wala hakusimama katika kweli kwa kuwa kweli hamna ndani yake. Asemapo uwongo, husema yaliyo yake mwenyewe, kwa sababu yu mwongo, na baba ya huo.


Ewe mwenye kujaa hila na uovu wote, mwana wa shetani, adui wa haki yote, huachi kuzipotoa njia za Bwana zilizonyoka?


na kumugojea Mwana wake kutoka mbinguni, ambae alimfufua katika wafu, Yesu, anaetuokoa na ghadhabu itakayokuja.


illi kwa vitu viwili visivyoweza kubadilika, ambavyo katika hivyo Mungu bawezi kusema nwongo, tupate faraja lililo imara, sisi tuliokimbilia kuyashika matumaini yale yawekwayo mbele yetu;


afanyae dhambi yu wa Shetani: kwa kuwa Shetani hutenda dhambi tangu mwanzo. Kwa kusudi hili Mwana wa Mungu alidhihiri, illi azivunje kazi za Shetani.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo