Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Luka 3:22 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

22 Roho Mtakatifu akashuka juu yake kwa mfano wa kiwiliwili kama hua, sauti ikatoka mbinguni, Wewe ndiwe mwana wangu, mpendwa wangu, ndiwe unipendezae.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

22 na Roho Mtakatifu akamshukia akiwa na umbo kama la njiwa. Sauti ikasikika kutoka mbinguni: “Wewe ndiwe Mwanangu mpendwa, nimependezwa nawe.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

22 na Roho Mtakatifu akamshukia akiwa na umbo kama la njiwa. Sauti ikasikika kutoka mbinguni: “Wewe ndiwe Mwanangu mpendwa, nimependezwa nawe.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

22 na Roho Mtakatifu akamshukia akiwa na umbo kama la njiwa. Sauti ikasikika kutoka mbinguni: “Wewe ndiwe Mwanangu mpendwa, nimependezwa nawe.”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

22 Roho Mtakatifu wa Mungu akashuka juu yake kwa umbo kama la hua, nayo sauti kutoka mbinguni ikasema: “Wewe ni Mwanangu mpendwa; nami nimependezwa nawe sana.”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

22 Roho wa Mwenyezi Mungu akashuka juu yake kwa umbo kama la hua, nayo sauti kutoka mbinguni ikasema: “Wewe ni Mwanangu mpendwa; nami nimependezwa nawe sana.”

Tazama sura Nakili




Luka 3:22
21 Marejeleo ya Msalaba  

Tazama, mtumishi wangu niiliyemteua; Mpendwa wangu, ambae moyo wangu umependezwa nae; Nitamtia roho yangu, Nae atuwatangazia Mataifa hukumu.


Alipokuwa akisema, wingu jeupe likawatia uvuli; sauti ikatoka katika lile wingu, ikinena, Huyu ni Mwanangu, mpendwa wangu, niliyependezwa nae; msikieni yeye.


Amemtegemea Mungu; na amwokoe sasa, kamii akimtaka; kwa maana alisema, Mimi ni Mwana wa Mungu.


Ndipo Yesu akafika hatta Yordani kwa Yohana kutoka Galilaya illi abatizwe nae.


Nae Yesu alipokwisha kubatizwa marra akapanda kutoka majini: mbingu zikamfunukia, akamwona Roho ya Mungu akishuka kama hua, akija juu yake:


na sauti toka mbinguni ikinena, Huyu ni Mwanangu, mpendwa wangu, ninaependezwa nae.


sauti ikatoka mbinguni, Wewe ndiwe Mwana wangu mpendwa, ndiwe unipendezae.


Tena, siku zile, alikuja Yesu kutoka Nazareti ya Galilaya, akabatizwa na Yohana katika Yardani.


Likawako wingu, likawatia uvuli: sauti ikatoka katika lile wingu, Huyu ui Mwana wangu, mpendwa wangu, msikieni yeye.


Utukufu una Mungu palipo juu, Na katika inchi amani, kwa watu aliowaridhia.


Akaanza kuwaambia, Leo andiko hili limetimia masikioni mwenu.


Yohana akashuhudu, akasema, Nimemwona Roho akishuka, kama hua, kutoka mbinguni; akakaa juu yake.


Bassi ikaja sauti kutoka mbinguni, Nimelitukuza, nami nitalitukuza tena.


Nae Baba aliyenipeleka amenishuhudia. Sauti yake hamkuisikia wakati wo wote, wala sura yake hamkuiona.


khabari za Yesu wa Nazareti, jinsi Mungu alivyomtia mafuta kwa Roho Mtakatifu na uguvu: nae akatembea huko na huko, akitenda kazi njema na kuponya wote walioonewa na Shetani; kwa maana Mungu alikuwa pamoja nae.


aliyetuokoa na uguvu za giza, akatuhamisha na kutuingiza katika ufalme wa Mwana wa pendo lake;


Mkimwendea yeye, jiwe lililo hayi, lililokataliwa na wana Adamu, bali kwa Mungu ni teule, lenye thamani,


Tufuate:

Matangazo


Matangazo