Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Luka 3:16 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

16 Yohana akajibu, akawaambia wote, Mimi nawabatiza kwa maji, lakini yuaja aliye hodari kuliko mimi, ambae kwamba mimi sistahili kumfungulia ukanda wa viatu vyake; yeye atawabatizeni kwa Roho Mtakatifu na kwa moto:

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

16 Hapo Yohane akawaambia wote, “Mimi ninawabatiza kwa maji, lakini anakuja mwenye uwezo kuliko mimi ambaye sistahili hata kumfungulia kamba za viatu vyake. Yeye atawabatizeni kwa Roho Mtakatifu na kwa moto.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

16 Hapo Yohane akawaambia wote, “Mimi ninawabatiza kwa maji, lakini anakuja mwenye uwezo kuliko mimi ambaye sistahili hata kumfungulia kamba za viatu vyake. Yeye atawabatizeni kwa Roho Mtakatifu na kwa moto.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

16 Hapo Yohane akawaambia wote, “Mimi ninawabatiza kwa maji, lakini anakuja mwenye uwezo kuliko mimi ambaye sistahili hata kumfungulia kamba za viatu vyake. Yeye atawabatizeni kwa Roho Mtakatifu na kwa moto.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

16 Yahya akawajibu akawaambia, “Mimi nawabatiza kwa maji. Lakini atakuja aliye na nguvu kuliko mimi, ambaye sistahili hata kufungua kamba za viatu vyake. Yeye atawabatiza kwa Roho wa Mungu na kwa moto.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

16 Yahya akawajibu, akawaambia, “Mimi nawabatiza kwa maji. Lakini atakuja aliye na nguvu kuniliko mimi, ambaye sistahili hata kufungua kamba za viatu vyake. Yeye atawabatiza kwa Roho wa Mwenyezi Mungu na kwa moto.

Tazama sura Nakili




Luka 3:16
24 Marejeleo ya Msalaba  

Mimi nawabatizeni katika maji mpate kutubu: bali yeye ajae nyuma yangu ni hodari kuliko mimi, wala sistahili hatta kuchukua viatu vyake; yeye atawabatizeni kwa Roho Mtakatifu na kwa moto.


Pepeto lake li mkononi mwake, nae ataitakasa sana sakafu yake; atakusanya nganu yake ghalani, bali makapi atayateketeza kwa moto usiozimika.


Yohana akawajibu akanena, Mimi nabatiza kwa maji: kati mwenu amesimama msiyemjua ninyi.


Ndiye ajae nyuma yangu, aliyekuwa mbele yangu, wala mimi sistahili niilegeze gidam ya kiatu chake.


Nami sikumjua, lakini yeye aliyenipeleka kubatiza kwa maji, huyu aliniambia, Yeye ambae utakaemwona Roho akishuka na kukaa juu yake, huyu ndiye abatizae kwa Roho Mtakatifu.


Aniaminiye mimi, kama maandiko yalivyonena, mito ya maji ya uzima itamtoka tumhoni.


ya kwamba Yohana alibatiza kwa maji, bali ninyi mtabatizwa katika Roho Mtakatifu baada ya siku hizi si nyingi.


Petro alipokuwa akisema maueno haya Roho Mtakatifu akawashukia wote waliosikia maneno yake.


Bassi akiisha kupandishwa hatta mkono wa kuume wa Mungu, na kupokea kwa Baba ile ahadi ya Roho Mtakatifu amekimwaga kitu hiki mnachokiona sasa na kukisikia.


Kwa maana katika Roho mmoja sisi sote tulibatizwa tukaingia katika mwili mmoja, ikiwa tu Wayahudi, au ikiwa tu Wayunani; ikiwa tu watumwa au ikiwa tu huru; nasi sote tulinyweshwa Roho mmoja.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo