Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Luka 3:1 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

1 HATTA katika mwaka wa kumi na tano wa kutawala kwake Tiberio Kaisari, Pontio Pilato alipokuwa liwali wa Yahudi, na Herode tetrarka wa Galilaya, na Filipo ndugu yake tetrarka wa Iturea, na wa inchi ya Trakoniti, na Lusania tetrarka wa Abilene,

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

1 Mwaka wa kumi na tano wa utawala wa Kaisari Tiberio, Pontio Pilato alikuwa anatawala mkoa wa Yudea. Herode alikuwa mtawala wa Galilaya, na ndugu yake Filipo alikuwa mtawala wa eneo la Iturea na Trakoniti. Lusania alikuwa mtawala wa Abilene,

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

1 Mwaka wa kumi na tano wa utawala wa Kaisari Tiberio, Pontio Pilato alikuwa anatawala mkoa wa Yudea. Herode alikuwa mtawala wa Galilaya, na ndugu yake Filipo alikuwa mtawala wa eneo la Iturea na Trakoniti. Lusania alikuwa mtawala wa Abilene,

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

1 Mwaka wa kumi na tano wa utawala wa Kaisari Tiberio, Pontio Pilato alikuwa anatawala mkoa wa Yudea. Herode alikuwa mtawala wa Galilaya, na ndugu yake Filipo alikuwa mtawala wa eneo la Iturea na Trakoniti. Lusania alikuwa mtawala wa Abilene,

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

1 Katika mwaka wa kumi na tano wa utawala wa Kaisari Tiberio, Pontio Pilato akiwa mtawala wa Yudea, Herode akiwa mfalme wa Galilaya, Filipo ndugu yake akiwa mfalme wa Iturea na nchi ya Trakoniti, na Lisania akiwa mfalme wa Abilene,

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

1 Katika mwaka wa kumi na tano wa utawala wa Kaisari Tiberio, Pontio Pilato akiwa mtawala wa Uyahudi, Herode akiwa mfalme wa Galilaya, Filipo ndugu yake akiwa mfalme wa Iturea na nchi ya Trakoniti, na Lisania akiwa mfalme wa Abilene,

Tazama sura Nakili




Luka 3:1
19 Marejeleo ya Msalaba  

WAKATI ule Herode tetrarka alisikia khabari za Yesu,


Maana Herode alikuwa amemkamata Yohana, akamfunga, akamtia gerezani, kwa ajili ya Herodias, mke wa Filipo ndugu yake.


Hatta panapo siku kuu ya kuzaliwa kwake Herode, binti Herodias alicheza kati ya watu, akampendeza Herode.


Bassi utuambie, Waonaje? Ni halali kumpa Kaisari kodi, au si halali?


wakamfunga, wakamchukua, wakampeleka kwa liwali Pontio Pilato.


Kwa maana Herode mwenyewe alikuwa ametuma wata, akamkamata Yohana, akamfunga gerezani, kwa ajili va Herodias, nikewe Filipo ndugu yake: kwa kuwa amemwoa; bassi Yohana alimwambia Herode,


Hatta ilipotokea siku ya kufaa, na Herode (siku kuu ya kuzaliwa kwake) alipowafanyia karamu masheki na majemadari na watu wakubwa wa Galilaya,


Siku ile ile baadhi ya Mafarisayo wakamwendea, wakamwambia, Ondoka hapa, ukaende zako: kwa maana Herode anataka kukuua.


HATTA siku zile kulitoka amri kwa Kaisari Augusto ya kama iandikwe orodha ya majina ya walimwengu wote:


Pilato akakata maneno yafanyike waliyoyataka.


Lakini Herode tetrarka, akikaripiwa nae kwa ajili ya Herodias, mke wa Filipo, ndugu yake, na kwa ajili ya maovu yote aliyoyafanya Herode,


Hatta Herode tetrarka akasikia yote yaliyotendwa nae, akaona mashaka, kwa kuwa wengine walisema kwamba Yohana amefufuka katika wafu:


Klaudio Lusia kwa liwali il aziz Feliki salamu!


Na miaka miwili ilipotimia. Feliki akampokea Porkio Festo atawale badala yake. Na Feliki, akitaka kuwafanyia Wayahudi fadhili, akamwacha Paolo amefungwa.


Na alipokwisha kusema haya mfalme na liwali na Bereniki na wale walioketi pamoja nao wakasimama,


Maana ni kweli, Herode na Pontio Pilato pamoja na mataifa na watu wa Israeli, walikusanyika juu ya mtumishi wako mtakatifu Yesu, uliyemtia mafuta,


Tufuate:

Matangazo


Matangazo