Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Luka 24:44 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

44 Akawaambia, Haya ndiyo maneno yangu niliyowaambieni, nilipokuwa kwenu, ya kuwa hayana buddi kutimizwa yote niliyoandikiwa katika torati ya Musa, na katika manabii, na katika zaburi.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

44 Halafu akawaambia, “Hii ndiyo maana ya maneno niliyowaambia nilipokuwa pamoja nanyi: Kwamba ilikuwa lazima kukamilisha yote yaliyoandikwa juu yangu katika sheria ya Mose na katika vitabu vya manabii na katika kitabu cha Zaburi.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

44 Halafu akawaambia, “Hii ndiyo maana ya maneno niliyowaambia nilipokuwa pamoja nanyi: Kwamba ilikuwa lazima kukamilisha yote yaliyoandikwa juu yangu katika sheria ya Mose na katika vitabu vya manabii na katika kitabu cha Zaburi.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

44 Halafu akawaambia, “Hii ndiyo maana ya maneno niliyowaambia nilipokuwa pamoja nanyi: kwamba ilikuwa lazima kukamilisha yote yaliyoandikwa juu yangu katika sheria ya Mose na katika vitabu vya manabii na katika kitabu cha Zaburi.”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

44 Akawaambia, “Haya ndio yale niliyowaambia nilipokuwa bado niko pamoja nanyi, kwamba yote yaliyoandikwa kunihusu katika Torati ya Musa, Manabii na Zaburi hayana budi kutimizwa.”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

44 Akawaambia, “Haya ndiyo yale niliyowaambia nilipokuwa bado niko pamoja nanyi, kwamba yote yaliyoandikwa kunihusu mimi katika Torati ya Musa, Manabii na Zaburi hayana budi kutimizwa.”

Tazama sura Nakili




Luka 24:44
88 Marejeleo ya Msalaba  

Haya yote yamekuwa, illi litimie neno lililonenwa na Bwana kwa ujumbe wa nabii akinena,


Toka wakati huo Yesu akaanza kuwaonya wanafunzi wake ya kwamba imempasa kwenda Yerusalemi, na kuteswa mengi na wazee na makuhani wakuu, na waandishi, na kuuawa, na siku ya tatu kufufuka.


Yatatimizwaje bassi maandiko, kwamba hivyo ndivyo vilivyopasa kuwa?


Lakini jambo hili lote limekuwa, illi maandiko ya manabii yatimizwe. Ndipo wanafunzi wake wote wakamwacha, wakakimbia.


Kwa sababu alikuwa akiwafundisha wanafunzi wake, akiwaambia ya kwamba Mwana wa Adamu anakwenda kutiwa katika mikono ya watu, nao watamwua; hatta akiisha kuuawa, baada ya siku tatu atafufuka.


Kwa sababu hizi ni siku ya mapatilizo, yote yaliyoandikwa yapate kutimizwa.


Kwa maana nawaambieni, Hili lililoandikwa halina buddi kutimizwa kwangu, Alihesabiwa pamoja na maasi; kwa maana linipasalo lina mwisho.


Akawaambia, Ndivyo ilivyoandikwa, na ndivyo ilivyompasa Kristo kuteswa, na kufufuka siku ya tatu;


Akawaagiza na kuwaamuru wasimwambie mtu neno hili, akisema, Imempasa Mwana wa Adamu kupata mateso mengi na kukataliwa na wazee na makuhani wakuu, na waandishi, na kuuawa, na siku ya tatu kufufuka.


Yawekeni maneno haya masikioni mwenu: kwa maana Mwana wa Adamu anakwenda kutiwa katika mikono ya watu.


Na kama Musa alivyomwinua nyoka jangwani, vivyo hivyo Mwana wa Adamu hana buddi kuinuliwa:


Mwayachunguza maandiko, kwa sababu mnadhani kwamba ninyi mna uzima wa milele ndani yake: na hayo ndiyo yanayonishuhudia:


Kwa maana kama mngalimwamini Musa, mngeniamini mimi; maana yeye aliandika khahari zangu.


kama ilivyoandikwa katika Zaburi ya pili, Wewe ndiwe Mwana wangu, mimi leo nimekuzaa.


Angalieni, bassi, isije khabari ile iliyonenwa katika manabii,


Kwa maana hutaniacha roho yangu katika kuzimu: Wala hutamtoa Mtakatifu wako aone uharibifu.


Lakini mambo yale aliyokhubiri Mungu tangu zamani kwa vinywa vya manabii wake wote, ya kama Kristo atateswa, ameyatimiza hivyo.


Musa huyo ndiye aliyewaambia wana wa Israeli, Bwana Mungu wenu atawainulieni nabii katika ndugu zenu, kama mimi: mtamsikia huyo.


BASSI kwa kuwa torati ni kivuli cha mema yatakayokuwa, wala si sura yenyewe ya mambo, kwa dhahihu zile zile wanazozitoa killa mwaka daima, hawawezi wakati wo wote kuwakamilisha wakaribiao.


Na Musa alikuwa mwaminifu katika nyumba yake yote kama mtumishi, awe ushuhuda wa mambo yatakayonenwa;


KWA maana Meikizedeki huyo, mfalme wa Salemi, kuhani wa Mungu aliye juu, aliyekutana na Ibrahimu baada ya kuwapiga wafalme, alimbariki;


Roho Mtakatifu akionyesha neno hili, ya kwamba njia ya kupaingia patakatifu ilikuwa haijadhihirishwa bado, hapo khema ya kwanza ilipokuwa ingali ikisimama.


wakitafuta ni wakati upi, na wakati wa namna gani ulioonywa na Roho ya Kristo iliyokuwa ndaui yao, aliyetangulia kuyashuhudia mateso yatakayompata Kristo, na utukufu utakaokuwa baada ya hayo.


Nikaanguka mbele ya miguu yake, nimsujudie, akaniambia, Angalia, usifanye hivi: mimi mjoli wako na mmoja wa ndugu zako walio na ushuhuda wa Yesu. Msujudu Mungu: kwa maana ushuhuda wa Yesu ni roho ya unabii.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo