Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Luka 24:32 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

32 Wakaambiana, Je! Mioyo yetu haikuwa ikiwaka ndani yetu, alipokuwa akisema nasi njiani, akitufunulia maandiko?

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

32 Basi, wakaambiana, “Je, mioyo yetu haikuwa inawaka ndani yetu wakati alipokuwa anatufafanulia Maandiko Matakatifu kule njiani?”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

32 Basi, wakaambiana, “Je, mioyo yetu haikuwa inawaka ndani yetu wakati alipokuwa anatufafanulia Maandiko Matakatifu kule njiani?”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

32 Basi, wakaambiana, “Je, mioyo yetu haikuwa inawaka ndani yetu wakati alipokuwa anatufafanulia Maandiko Matakatifu kule njiani?”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

32 Wakaulizana wao kwa wao, “Je, mioyo yetu haikuwaka ndani yetu alipokuwa anazungumza nasi njiani na kutufafanulia Maandiko?”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

32 Wakaulizana wao kwa wao, “Je, mioyo yetu haikuwakawaka kwa furaha ndani yetu alipokuwa anazungumza nasi njiani na kutufafanulia Maandiko?”

Tazama sura Nakili




Luka 24:32
14 Marejeleo ya Msalaba  

wala pasipo mfano hakusema nao: akawaeleza wanafunzi wake mambo yote kwa faragha.


Ndipo akaamsha akili zao, wapate kuyatambua maandiko matakatifu.


Roho ndiyo itiayo uzima; mwili haufai kitu; maneno ninayowaambieni ni roho, tena ni uzima.


Wakiislia kuwekana kwa siku, wakaja kwake nyumbani kwake, watu wengi sana, akawaeleza kwa taratibu na kuushuhudia ufalme wa Mungu, akiwaonya mambo yake Yesu, kwa maneno ya sharia ya Musa na ya manabii, tangu assubuhi hatta jioni.


Maana Neno la Mungu li hayi, tena lina nguvu, tena lina ukali kuliko ukali wa upanga ukatao kuwili, tena lachoma kiasi cha kuzigawanya nafsi na roho, na viungo na mafuta yaliyomo ndani yake; li jepesi kuyatambua mawazo na makusudi ya moyo.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo