Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -

Luka 23:8 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

8 Na Herode alipomwona Yesu, akafurahiwa sana: kwa kuwa tangu zamani alikuwa akitaka kumwona, kwa sababu amesikia mambo yake; akataraja kuona ishara inafanyika nae.

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

8 Herode alifurahi sana alipomwona Yesu. Alikuwa amekwisha sikia habari zake, na hivyo alikuwa anatazamia kwa muda mrefu kumwona kwa macho yake mwenyewe. Zaidi ya hayo, alikuwa anatumaini kumwona Yesu akitenda mwujiza.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

8 Herode alifurahi sana alipomwona Yesu. Alikuwa amekwisha sikia habari zake, na hivyo alikuwa anatazamia kwa muda mrefu kumwona kwa macho yake mwenyewe. Zaidi ya hayo, alikuwa anatumaini kumwona Yesu akitenda mwujiza.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

8 Herode alifurahi sana alipomwona Yesu. Alikuwa amekwisha sikia habari zake, na hivyo alikuwa anatazamia kwa muda mrefu kumwona kwa macho yake mwenyewe. Zaidi ya hayo, alikuwa anatumaini kumwona Yesu akitenda mwujiza.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

8 Herode alipomwona Isa alifurahi sana, kwa sababu kwa muda mrefu alikuwa amesikia mambo mengi kumhusu. Pia alitarajia kumwona akifanya miujiza kadha wa kadha.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

8 Herode alipomwona Isa alifurahi sana, kwa sababu kwa muda mrefu alikuwa amesikia mambo mengi kumhusu yeye. Pia alitarajia kumwona akifanya miujiza kadha wa kadha.

Tazama sura Nakili

Luka 23:8
8 Marejeleo ya Msalaba  

WAKATI ule Herode tetrarka alisikia khabari za Yesu,

Mfalme Herode akasikia khabari; kwa maana jina lake limepata kutangaa, akanena, Yohana Mbatizaji amefufuka, na kwa hiyo nguvu hizi zinatenda kazi ndani yake. Wengine walinena, Yu Eliya.

Akawaita makutano na wanafunzi wake, akawaambia, Atakae kuniandama na ajikane nafsi yake, ajitwike msalaba wake, anifuate.

Akawaambia, Hapana shaka mtaniambia methali hii, Tabibu, jiponye nafsi yako: mambo yote tuliyosikia yametendeka Kapernaum, yatende na hapa pia katika inchi yako mwenyewe.

Nipe na mimi uwezo huu, illi killa mtu nitakaemweka mikono yangu, apokee Roho Mtakatifu.

Tufuate:

Matangazo

Matangazo