Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Luka 23:51 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

51 (mtu huyu hakuwa akikubali shauri lao wala tendo lao), mwenyeji wa Arimathaya, mji wa Wayahudi, nae mwenyewe akiutazamia ufalme wa Mungu.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

51 Alikuwa akitazamia kuja kwa ufalme wa Mungu. Ingawa alikuwa mmoja wa Baraza Kuu la Wayahudi, hakuwa amekubaliana nao katika kitendo chao.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

51 Alikuwa akitazamia kuja kwa ufalme wa Mungu. Ingawa alikuwa mmoja wa Baraza Kuu la Wayahudi, hakuwa amekubaliana nao katika kitendo chao.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

51 Alikuwa akitazamia kuja kwa ufalme wa Mungu. Ingawa alikuwa mmoja wa Baraza Kuu la Wayahudi, hakuwa amekubaliana nao katika kitendo chao.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

51 lakini yeye hakuwa amekubaliana na maamuzi na vitendo vya viongozi wenzake. Huyu alikuwa raia wa Arimathaya huko Yudea, naye alikuwa anaungojea ufalme wa Mungu kwa matarajio makubwa.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

51 lakini yeye hakuwa amekubaliana na maamuzi na vitendo vya viongozi wenzake. Huyu alikuwa mwenyeji wa Arimathaya huko Uyahudi, naye alikuwa anaungojea Ufalme wa Mwenyezi Mungu kwa matarajio makubwa.

Tazama sura Nakili




Luka 23:51
13 Marejeleo ya Msalaba  

Ilipokuwa jioni akafika mtu tajiri wa Arimathaya, jina lake Yusuf, nae mwenyewe alikuwa mwanafunzi wa Yesu;


akaenda Yusuf, mtii wa Arimathaya, mstahiki, mtu wa baraza la mashauri, nae mwenyewe anautazamia ufalme wa Mungu; akafanya ujasiri, akaingia mbele ya Pilato akauomba mwili wake Yesu.


Bassi kulikuwako mtu katika Yerusalemi, jina lake Sumeon; na yule mtu mwenye haki, mtawa, akitazamia faraja ya Israeli: na Roho Mtakatifu alikuwa pamoja nae.


Akitokea yeye nae saa ileile, alimshukuru Mungu, akawapasha khabari zake watu wote waliokuwa wakitazamia ukombozi katika Yerusalemi.


Akamwambia Yesu, Bwana, unikumbuke ujapo katika ufalme wako.


Bassi mtu huyu akamwendea Pilato akaomba apewe mwili wa Yesu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo