Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Luka 23:34 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

34 Yesu akasema, Baba, uwasamehe, kwa maana hawajui watendalo. Wakagawanya nguo zake, wakipiga kura.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

34 Yesu akasema, “Baba, uwasamehe kwa maana hawajui wanalofanya.” Kisha wakagawana mavazi yake kwa kuyapigia kura.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

34 Yesu akasema, “Baba, uwasamehe kwa maana hawajui wanalofanya.” Kisha wakagawana mavazi yake kwa kuyapigia kura.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

34 Yesu akasema, “Baba, uwasamehe kwa maana hawajui wanalofanya.” Kisha wakagawana mavazi yake kwa kuyapigia kura.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

34 Isa akasema, “Baba, wasamehe, kwa maana hawajui walitendalo!” Wakagawana nguo zake kwa kupiga kura.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

34 Isa akasema, “Baba, wasamehe, kwa maana hawajui walitendalo!” Wakagawana nguo zake kwa kupiga kura.

Tazama sura Nakili




Luka 23:34
26 Marejeleo ya Msalaba  

Wakati ule Yesu akajibu akasema, Nakushukuru, Baba, Bwana wa mbingu na inchi, kwa kuwa uliwaficha haya wenye hekima na busara, ukawafunulia wadogo:


Naam, Baba, kwa kuwa ndivyo ilivyopendeza mbele yako.


bali mimi nawaambieni, Wapendeni adui zenu, wabarikini wanaowalaani, watendeni mema wanaowachukia, waombeeni wanaowatendea ukorofi, na kuwatesa;


Wakamsulibi, wakagawanya nguo zake wakizipigia kura killa mtu atwae nini.


Baba, ukipenda, uniondolee kikombe hiki: lakini si kama nitakavyo mimi, illa utakavyo wewe vifanyike.


Mimi nawaombea hao; siuombei ulimwengu, bali wao ulionipa, kwa kuwa hao ni wako.


Yesu akamjibu, Usingekuwa na mamlaka yo yote, kama usingepewa toka juu: kwa sababu hii yeye aliyenitia mikononi mwako yuna dhambi iliyo kubwa zaidi.


Paolo akapaaza sauti yake kwa uguvu, akisema, Usijidhuru, kwa maana sisi sote tupo hapa.


Bassi sasa ndugu, najua ya kuwa mliyatenda haya kwa kutokujua kwenu, kama na wakuu wenu walivyotenda.


Akapiga magoti, akalia kwa sauti kuu, Bwana, usiwahesabie dhambi hii. Akiisha kusema haya akalala.


Wabarikini wanaowafukuzeni; barikini, wala msilaani.


ambayo wenye kutawala dunia hii hawakuijua hatta mmoja; maana kama wangaliijua, wasingalimsulibisha Bwana wa utukufu;


tena twataabika tukifanya kazi kwa mikono yetu wenyewe. Tukitukanwa twabariki, tukiudhiwa twavumilia;


mimi niliyekuwa kwanza mtukanaji, mwenye kuudhi watu, mwenye jeuri: lakini nalirehemiwa kwa kuwa nalitenda hivyo kwa njinga, na kwa kutokuwa na imani;


watu wasiolipa baya badala ya baya, au laumu badala ya laumu; bali wabarikio; kwa sababu ndiyo mlioitiwa illi mrithi baraka.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo