Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Luka 23:26 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

26 Walipokuwa wakimchukua, wakamshika Mkurene Simon, aliyekuwa akitoka shamba, wakamtwika yeye msalaba, auchukue nyuma yake Yesu.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

26 Walipokuwa wakimpeleka, walikutana na mtu mmoja aitwaye Simoni wa Kurene, aliyekuwa anatoka shambani. Basi, walimkamata, wakamtwika ule msalaba auchukue nyuma ya Yesu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

26 Walipokuwa wakimpeleka, walikutana na mtu mmoja aitwaye Simoni wa Kurene, aliyekuwa anatoka shambani. Basi, walimkamata, wakamtwika ule msalaba auchukue nyuma ya Yesu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

26 Walipokuwa wakimpeleka, walikutana na mtu mmoja aitwaye Simoni wa Kurene, aliyekuwa anatoka shambani. Basi, walimkamata, wakamtwika ule msalaba auchukue nyuma ya Yesu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

26 Walipokuwa wakienda naye, wakamkamata mtu mmoja aitwaye Simoni Mkirene, aliyekuwa anapita zake kuingia mjini kutoka shambani. Wakambebesha msalaba, wakamlazimisha auchukue nyuma ya Isa.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

26 Walipokuwa wakienda naye, wakamkamata mtu mmoja aitwaye Simoni mwenyeji wa Kirene, aliyekuwa anapita zake kuingia mjini kutoka shambani. Wakambebesha msalaba, wakamlazimisha auchukue nyuma ya Isa.

Tazama sura Nakili




Luka 23:26
11 Marejeleo ya Msalaba  

Na mtu atakaekutumikisha maili moja, nenda nae mbili.


Na mfu ye yote asiyechukua msalaba wake na kuja nyuma yangu, hawezi kuwa mwanafunzi wangu.


Akamfungua yeye aliyetiwa gerezani kwa fitina na uuaji, waliyemtaka: akatoa Yesu kwa mapenzi yao.


Akawaamhia wote, Atakae kuniandama, na ajikane nafsi yake, ajitwike msalaba wake killa siku, anifuate.


NA huko Antiokia katika kanisa lililokuwako palikuwa na manabii na waalimu, Barnaba na Sumeon aitwae Niger, na Lukio Mkurene, na Manaen aliyekuwa ndugu wa kunyonya wa Herode mfalme, na Saul.


Frugia na Pamfulia, Misri na pande za Libua karibu na Kurene, na Warumi wageni, Wayahudi na Waongofu,


Wakawaweka mbele ya mitume, na walipokwisha kuomba wakaweka mikono yao juu yao.


Lakini baadhi ya watu wa sunagogi lililokwitwa sunagogi la Malibertino, na la Wakurene na la Waiskanderia, na la wale wa Kilikia na Asia, wakaondoka wakajadiliana na Stefano:


Tufuate:

Matangazo


Matangazo