Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Luka 23:14 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

14 Mmeniletea mtu huyu, kana kwamba anapotosha watu; nami hassi nilipomhukumu mbele yenu, sikuona khatiya katika mtu huyu katika yale mliyomshitaki;

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

14 akawaambia, “Mmemleta mtu huyu kwangu mkisema kwamba alikuwa anawapotosha watu. Sasa sikilizeni! Baada ya kuchunguza jambo hilo mbele yenu, sikumpata na kosa lolote kuhusu mashtaka yenu juu yake.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

14 akawaambia, “Mmemleta mtu huyu kwangu mkisema kwamba alikuwa anawapotosha watu. Sasa sikilizeni! Baada ya kuchunguza jambo hilo mbele yenu, sikumpata na kosa lolote kuhusu mashtaka yenu juu yake.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

14 akawaambia, “Mmemleta mtu huyu kwangu mkisema kwamba alikuwa anawapotosha watu. Sasa sikilizeni! Baada ya kuchunguza jambo hilo mbele yenu, sikumpata na kosa lolote kuhusu mashtaka yenu juu yake.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

14 akawaambia, “Ninyi mlimleta huyu mtu kwangu kana kwamba ni mtu anayewachochea watu ili waasi. Nimemhoji mbele yenu nami sikupata msingi wowote wa mashtaka yenu dhidi yake.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

14 akawaambia, “Ninyi mlimleta huyu mtu kwangu kana kwamba ni mtu anayewachochea watu ili waasi. Nimemhoji mbele yenu nami nimeona hakuna msingi wowote wa mashtaka yenu dhidi yake.

Tazama sura Nakili




Luka 23:14
10 Marejeleo ya Msalaba  

Na alipokuwa ameketi juu ya kiti cha hukumu, mkewe alimpelekea mjumbe, kumwambia, Usiwe na neno na yule mwenye haki: kwa sababu nimeteswa mengi leo katika udoto kwa ajili yake.


Pilato alipoona ya kuwa hafai neno, bali ya kuwa inazidi kuwa ghasia, akatwaa maji, akanawa mikono yake mbele ya makutano, akasema, Mimi sina khatiya kwa khabari ya damu ya mtu huyu mwenye haki: tazameni hayo ninyi wenyewe.


akinena, Nalikosa nilipoisaliti damu isiyo na khatiya. Wakanena, Bassi, haya yatukhussu nini sisi? Tazama wewe hayo.


Bassi yule akida, nao walio pamoja nae wakimwangalia Yesu, walipoliona tetemeko la inchi na mambo yaliyofanyika, wakaogopa sana, wakinena, Hakika huyu alikuwa Mwana wa Mungu.


Na wasipopata sababu ya kumfisha wakamwomba Pilato auawe.


Watu hawa walikuwa waungwana kuliko wale wa Thessaloniki, kwa kuwa walilipokea Neno kwa uelekefu wa moyo, wakayachunguza maandiko, waone kwamba mambo hayo ndivyo yalivyo.


Maana ilipendeza sisi tuwe na kuhani mkuu wa namna hii, aliye mtakatifu, asiokuwa na uovu, asiokuua na waa lolote, aliyetengwa na wakosaji, aliyekuwa juu kuliko mbingu;


Tufuate:

Matangazo


Matangazo