Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Luka 22:52 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

52 Yesu akawaambia waliomjia, makuhani wakuu, na majemadari wa hekalu, na wazee, Kama juu ya mnyanyangʼanyi mmetoka kwa panga na marungu?

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

52 Kisha Yesu akawaambia makuhani wakuu, wakubwa wa walinzi wa hekalu na wazee waliokuja kumkamata: “Je, mmekuja na mapanga na marungu kunikamata kana kwamba mimi ni mnyanganyi?

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

52 Kisha Yesu akawaambia makuhani wakuu, wakubwa wa walinzi wa hekalu na wazee waliokuja kumkamata: “Je, mmekuja na mapanga na marungu kunikamata kana kwamba mimi ni mnyanganyi?

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

52 Kisha Yesu akawaambia makuhani wakuu, wakubwa wa walinzi wa hekalu na wazee waliokuja kumkamata: “Je, mmekuja na mapanga na marungu kunikamata kana kwamba mimi ni mnyang'anyi?

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

52 Kisha Isa akawaambia wale viongozi wa makuhani, maafisa wa walinzi wa Hekalu, pamoja na wazee waliokuwa wamekuja kumkamata, “Mmekuja na panga na marungu, kana kwamba mimi ni mnyang’anyi?

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

52 Kisha Isa akawaambia wale viongozi wa makuhani, maafisa wa walinzi wa Hekalu, pamoja na wazee waliokuwa wamekuja kumkamata, “Mmekuja na panga na marungu, kana kwamba mimi ni mnyang’anyi?

Tazama sura Nakili




Luka 22:52
10 Marejeleo ya Msalaba  

Hatta alipokuwa akisema, Yuda, mmoja wa wale thenashara akaja, na pamoja nae makutano mengi, wana panga na marungu, wametoka kwa makuhani wakuu na wazee wa watu.


Saa ile Yesu akawaambia makutano, Je, mmetoka, mfano wa watu wafukuzao mnyangʼanyi mna panga na marungu, kunitwaa? Killa siku naliketi mbele zenu hekaluni, nikifundisha, wala hamkunikamata.


Kwa maana nawaambieni, Hili lililoandikwa halina buddi kutimizwa kwangu, Alihesabiwa pamoja na maasi; kwa maana linipasalo lina mwisho.


Akaenda zake akasema na makuhani wakuu na majemadari jinsi ya kumtia katika mikono yao.


Yesu akajibu, akasema, Acheni kadiri hii. Akamgusa sikio, akamponya.


Killa siku nilipokuwa pamoja nanyi hekaluni hamkuninyoshea mikono; lakini saa yenu hii, na mamlaka ya giza.


Nilipokuwa pamoja nao ulimwenguni, mimi naliwalinda kwa jina lako: wale ulionipa naliwatunza, wala hapana mmojawapo wao aliyepotea, illa yule mwana wa upotevu maandiko yapate kutimizwa.


Yule jemadari akaenda pamoja na watumishi, wakawaleta, lakini si kwa nguvu, kwa maana waliogopa watu wasije wakawatupia mawe.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo