Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Luka 22:3 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

3 Shetani akamwingia Yuda, aitwae Iskariote, nae alikuwa katika hesabu ya wale thenashara.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

3 Basi, Shetani akamwingia Yuda aitwaye Iskarioti, mmoja wa wale mitume kumi na wawili.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

3 Basi, Shetani akamwingia Yuda aitwaye Iskarioti, mmoja wa wale mitume kumi na wawili.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

3 Basi, Shetani akamwingia Yuda aitwaye Iskarioti, mmoja wa wale mitume kumi na wawili.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

3 Shetani akamwingia Yuda, aliyeitwa Iskariote, mmoja wa wale kumi na wawili.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

3 Shetani akamwingia Yuda, aliyeitwa Iskariote, mmoja wa wale Kumi na Wawili.

Tazama sura Nakili




Luka 22:3
16 Marejeleo ya Msalaba  

Simon Kananayo, na Yuda Iskariote, ndiye aliyemsaliti.


Akajibu, akasema, Yeye aliyetia mkono wake pamoja nami katika sahani, ndiye atakaenisaliti.


Ndipo Yesu akamwambia, Nenda zako, Shetani: kwa maana imeandikwa, Utamsujudia Bwana Mungu wako, nae peke yake utamwabudu.


Illa angalieni, mkono wake anisalitiye u pamoja nami mezani.


Yuda wa Yakobo; na Yuda Iskariote, ndiye aliyekuwa khaini.


Aliyasema haya, si kwa kuwahurumia maskini; hali kwa kuwa ni mwizi, nae ndiye aliyeshika mfuko, akavichikua vilivyotiwa humo.


Sisemi khabari za ninyi nyote: nawajua niliowachagua; lakini andiko lipate kutimizwa, Aulae mkate pamoja nami ameinua kisigino chake juu yangu.


Hatta wakati wa chakula cha jioni, Shetani alipokwisha kumtia Yuda, mwana wa Simon Iskariote, moyo wa kumsaliti,


Petro akamwambia, Anania, kwa nini Shetani amekujaza moyo kumwambia uwongo Roho Mtakatifu, na kuzuia kwa siri sehemu ya thamani ya uwanja?


Tufuate:

Matangazo


Matangazo