Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Luka 21:8 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

8 Akasema, Jibadharini, msidanganyike; kwa sababu wengi watakuja kwa jina langu, wakinena, Mimi ndiye, na, Majira yamekaribia. Bassi, msiwafuate hawo.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

8 Yesu akawajibu, “Jihadharini, msije mkadanganyika. Maana wengi watatokea na kulitumia jina langu, kila mmoja akidai kwamba yeye ni mimi, na kwamba wakati ule umekaribia. Lakini nyinyi msiwafuate!

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

8 Yesu akawajibu, “Jihadharini, msije mkadanganyika. Maana wengi watatokea na kulitumia jina langu, kila mmoja akidai kwamba yeye ni mimi, na kwamba wakati ule umekaribia. Lakini nyinyi msiwafuate!

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

8 Yesu akawajibu, “Jihadharini, msije mkadanganyika. Maana wengi watatokea na kulitumia jina langu, kila mmoja akidai kwamba yeye ni mimi, na kwamba wakati ule umekaribia. Lakini nyinyi msiwafuate!

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

8 Isa akawajibu, “Jihadharini msije mkadanganywa. Maana wengi watakuja kwa Jina langu, wakidai, ‘Mimi ndiye,’ na, ‘Wakati umekaribia.’ Msiwafuate.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

8 Isa akawajibu, “Jihadharini msije mkadanganywa. Maana wengi watakuja kwa Jina langu, wakidai, ‘Mimi ndiye,’ na, ‘Wakati umekaribia.’ Msiwafuate.

Tazama sura Nakili




Luka 21:8
26 Marejeleo ya Msalaba  

Na manabii wengi wa uwongo wataondoka, watadanganya wengi.


Tubuni; kwa maana ufalme wa mbinguni umekaribia.


Tokea wakati huo Yesu akaanza kukhubiri, na kusema, Tubuni, maana ufalme wa mbinguni umekaribia.


Na watawaambieni, Tazama huko, au tazama huko! Msiondoke hapo mlipo wala msiwafuate.


Wakuimwuliza, wakisema, Mwalimu, haya yatakuwa lini, bassi? Na nini dalili ya kuwa haya yote ni karibu ya kutimia?


Nanyi mtakaposikia khabari za vita na fitina msitishwe: maana haya hayana buddi kutukia kwanza, lakini mwisho wenyewe hauji marra moja.


Mimi nimekuja kwa jina la Baba yangu, nanyi hamnipokei: mwingine akija kwa jina lake mwenyewe mtampokea huyo.


Bassi naliwaambieni ya kwamba mtakufa katika dhambi zenu; kwa kuwa msipoamini ya kuwa mimi ndiye, mtakufa katika dhambi zenu.


Bassi Yesu akawaambia, Mtakapokuwa mmekwisha kumwinua Mwana wa Adamu, ndipo mtakapofahamu ya kuwa mimi ndiye, na ya kuwa sifanyi neno kwa nafsi yangu tu, illa kama Baba yangu alivyonifundisha, ndivyo nisemavyo.


Au hamjui ya kuwa wadhalimu hawataurithi ufalme wa Mungu? Msidanganyike. Waasharati hawataurithi ufalme wa Mungu, wala waabudu sanamu, wala wazinzi, wala wa kike, wala wafira,


Mtu asiwadanganye kwa maneno yasiyo maana; maana kwa sababu ya haya ghadhabu ya Mungu huwajia wana wa uasi.


Mtu aliye yote asiwadanganye kwa njia yo yote, maana haiji isipokuja kwanza ile faraka, akafumiliwa yule mtu wa dhambi, mwana wa uharibifu,


Lakini watu wabaya na wadanganyaji wataendelea na kuzidi kuwa waovu, wakidanganya na wakidanganyika.


WAPENZI, msiamini kiila rolio, bali zijaribuni roho, kwamba zimetokana na Mungu; kwa sababu manabii wa uwongo wengi wametokea duniani.


Kwa maana wadanganyifu wengi wameingia katika dunia, wasio-ungama ya kuwa Yesu Kristo yuaja katika mwili. Huyo ndiye yule mdanganyifu na adui wa Kristo.


Yu kheri asomae, nao wayasikiao maneno ya unabii huu na kuyafanya yaliyoandikwa humo: maana wakati ni karibu.


Joka akatupwa, yule mkubwa, nyoka wa zamani, aitwae Msingiziaji na Shetani, audanganyae ulimwengu wote; akatupwa hatta inchi, na malaika zake wakatupwa pamoja nae.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo