Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Luka 21:34 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

34 Bassi, jiangalieni, mioyo yenu isije ikalemewa na ulafi na ulevi, na masumbufu ya maisha haya,

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

34 “Muwe macho, mioyo yenu isije ikalemewa na anasa, ulevi na shughuli za maisha haya. La sivyo, siku ile itawajieni ghafla.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

34 “Muwe macho, mioyo yenu isije ikalemewa na anasa, ulevi na shughuli za maisha haya. La sivyo, siku ile itawajieni ghafla.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

34 “Muwe macho, mioyo yenu isije ikalemewa na anasa, ulevi na shughuli za maisha haya. La sivyo, siku ile itawajieni ghafla.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

34 “Jihadharini mioyo yenu isije ikalemewa na anasa, ulevi na fadhaa za maisha haya, nayo siku ile ikawakuta ninyi bila kutazamia kama mtego unasavyo.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

34 “Jihadharini mioyo yenu isije ikalemewa na anasa, ulevi na fadhaa za maisha haya, nayo siku ile ikawakuta ninyi bila kutazamia kama vile mtego unasavyo.

Tazama sura Nakili




Luka 21:34
37 Marejeleo ya Msalaba  

Nae aliyepandwa penye miiba, huyu ndiye alisikiae lile neno; na shughuli za dunia, na udanganyifu wa mali hulisonga lile neno, likawa halizai.


Nanyi jihadharini nafsi zenu; maana watawapelekeni maharazani: na katika masunagogi mtapigwa: na mtachukuliwa mbele za maliwali na wafalme kwa ajili yangu, kuwa ushuhuda kwao.


na shughuli za dunia, na udanganyifu wa mali, na tamaa za mambo mengine zikiingia, hulisonga lile neno, likawa halizai.


Bwana akamjibu akamwambia, Martha, Martha, unajisumbua na kujifadhaisha kwa ajili ya mambo mengi:


Na ninyi, bassi, mwe tayari, kwa sababu saa msiyodhani, Mwana wa Adamu yuaja.


Jihadharini: ndugu yako akikosa, mwonye; akitubu, msamehe,


siku ile ikawajieni kwa ghafula, kama mtego, maana hivyo ndivyo itakavyowajia watu wote wakaao juu ya uso wa dunia yote.


Akasema, Jibadharini, msidanganyike; kwa sababu wengi watakuja kwa jina langu, wakinena, Mimi ndiye, na, Majira yamekaribia. Bassi, msiwafuate hawo.


Nazo zilizoangukia miibani, hawa ndio waliosikia, nao wakienda zao husongwa na shughuli, na mali, na anasa za maisha, wasizae kwa utimilifu.


Lakini sasa nimewaandikieni kwamba msichangamane na mtu aitwae ndugu, akiwa mzinzi au mwenye kutamani an mwenye kuabudu sanamu au mtukanaji au mlevi au mnangʼanyi; mtu wa namna hii msikubali hatta kula nae.


wala wevi, wala watamanio, wala walevi, wala watukanaji, wala wanyangʼanyi.


ibada ya sanamu, uchawi, uadui, ugomvi, wivu, hasira, fitina, faraka, nzushi,


Msijisumbue kwa neno lo lote; bali katika killa neno kwa kusali na kuomba pamoja na kushukuru haja zenu zijulike kwa Mungu.


mkiangalia sana mtu asiipungukie neema ya Mungu; shina la uchungu lisije likachipuka na kuwasumbua watu wengi, wakatiwe najis kwa hilo.


Maana siku ya Bwana itakuja kama mwizi usiku; katika siku biyo mbingu zitatoweka kwa mshindo mkuu, na viumbe vya asili vitaunguzwa, na kufumuliwa, na inchi na kazi zilizomo ndani yake zitateketea.


Kwa hiyo, wapenzi, kwa kuwa mnatazamia hayo, fanyeni bidii illi muonekane kuwa hamna mawaa au aibu mbele yake, katika amani.


Bassi kumbuka jinsi ulivyopokea, na jinsi ulivyosikia; yashike hayo na kutubu. Illakini usipokesha nitakuja kwako kama mwizi, nawe hutaijua saa nitakayokuja kwako.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo