Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Luka 21:19 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

19 Kwa subira yenu mtazipata robo zenu.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

19 Kwa uvumilivu wenu, mtayaokoa maisha yenu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

19 Kwa uvumilivu wenu, mtayaokoa maisha yenu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

19 Kwa uvumilivu wenu, mtayaokoa maisha yenu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

19 Kwa kuvumilia mtaokoa roho zenu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

19 Kwa kuvumilia mtaokoa roho zenu.

Tazama sura Nakili




Luka 21:19
26 Marejeleo ya Msalaba  

Na mtakuwa mkichukiwa na watu wole kwa ajili ya jina langu: lakini adumuye hatta mwisho, ndiye atakaeokoka.


Lakini astahimiliye hatta mwisho, ndiye atakaeokoka.


Nazo penye udongo mwema, hawa ndio ambao kwamba kwa moyo mzuri na mwema hulisikia neno, wakalishika, wakazaa kwa saburi.


Kwa kuwa yote yaliyotangulia kuandikwa yaliandikwa kutufundisha sisi, illi kwa uvumilivu na faraja ya maandiko tupate kuwa na tumaini.


wale ambao kwa kustahimili katika kutenda mema wanatafuta utukufu na heshima na kutoa kuharibika, nzima wa milele;


Wala si hivyo tu, illa twafurahi katika mateso pia, tukijua ya kuwa dhiiki, kazi yake ni kuleta uvumilivu,


na kazi ya uvumilivu uthabiti wa moyo, na kazi ya uthabiti wa moyo tumaini,


Bali tukikitumaini kitu tusichokiona, twakingojea kwa uvumilivu.


wala hatuachi kuikumbuka kazi yenu ya amani, na taabu yenu ya upendo, na uvumilivu wenu wa tumaini lililo katika Bwana Yesu Kristo, mbele za Mungu Baba yetu;


Bwana awaongozeni mioyo yenu mkapate pendo la Mungu, na uvumilivu wa Kristo.


Maana mnahitaji uvumilivu, illi mkiisha kuyafanya mapenzi ya Mungu muipate abadi.


Nasi twataka killa mmoja wenu aidhihirishe bidii ile ile, kwa utimilifu wa matumaini hatta mwisho;


Na hivyo kwa kuvumilia akaipata ile ahadi.


mkifahamu ya kuwa kujaribiwa imani yenu huleta saburi.


Na saburi iwe na kazi kamilifu, mpate kuwa wakamilifu na watimilifu bila kupungukiwa neno.


na katika maarifa yenu kiasi, na katika kiasi chenu uvumilivu, na katika uvumilivu wenu utawa,


Mimi Yohana, ndugu yenu na mwenye kushiriki pamoja nanyi katika mateso na ufalme na uvumilivu wa Yesu Kristo, nalikuwa katika kisiwa kiitwacho Patmo, kwa ajili ya Neno la Mungu, na kwa ajili ya ushuhuda wa Yesu.


Mtu akichukua mateka achukuliwa mateka. Mtu akiua kwa upanga, atauawa kwa upanga. Hivyo ndivyo uvumilivu na imani ya watakatifu.


Hapo ndipo penye uvumilivu wa watakatifu wazishikao amri za Mungu, na imani ya Yesu.


Kwa kuwa ulilishika neno la uvumilivu wangu, mimi nami nitakulinda, utoke katika saa ya kujaribiwa iliyo tayari kuujia ulimwengu wote, kuwajaribu wakaao juu ya inchi.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo