Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Luka 2:46 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

46 Ikawa baada ya siku tatu, wakamwona hekaluni, ameketi kati ya waalimu, akiwasikiliza, na kuwauliza.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

46 Siku ya tatu, walimkuta hekaluni kati ya waalimu, akiwasikiliza na kuwauliza maswali.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

46 Siku ya tatu, walimkuta hekaluni kati ya waalimu, akiwasikiliza na kuwauliza maswali.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

46 Siku ya tatu, walimkuta hekaluni kati ya waalimu, akiwasikiliza na kuwauliza maswali.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

46 Baada ya siku tatu wakamkuta ndani ya Hekalu, akiwa ameketi katikati ya walimu wa Torati, akiwasikiliza na kuwauliza maswali.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

46 Baada ya siku tatu wakamkuta ndani ya Hekalu, akiwa ameketi katikati ya walimu wa Torati, akiwasikiliza na kuwauliza maswali.

Tazama sura Nakili




Luka 2:46
13 Marejeleo ya Msalaba  

Maana kama vile Yunus alivyokuwa siku tatu mchana na nsiku katika tumbo la nyamgumi, hivyo ndivyo Mwana wa Adamu atakavyokuwa siku tatu mchana na usiku katika moyo wa inchi.


Toka wakati huo Yesu akaanza kuwaonya wanafunzi wake ya kwamba imempasa kwenda Yerusalemi, na kuteswa mengi na wazee na makuhani wakuu, na waandishi, na kuuawa, na siku ya tatu kufufuka.


Wote waliomsikia wakataajahu kwa akili zake na majibu yake.


Hatta siku moja ya siku zile alikuwa akifundisha, na Mafarisayo na waandishi wameketi, waliokuwa wametoka katika killa kijiji cha Galilaya, na cha Yahudi, na Yerusalemi; uweza wa Bwana ulikuwa pamoja nae apate kuwaponya.


Yesu akajibu akamwambia, Je! Wewe u mwalimu katika Israeli, na haya huyafahamu?


Lakini mtu mmoja, Farisayo, jina lake Gamaliel, mwalimu wa torati, mwenye kuheshimiwa na watu wote, akasimama katika baraza,


wapenda kuwa waalimu wa sharia, wasiyafahamu wasemayo wala mambo yale wayanenayo kwa utbabiti.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo