Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -

Luka 2:4 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

4 Na Yusuf nae akaondoka Galilaya kutoka mji wa Nazareti, akapanda kwenda Yahudi hatta mji wa Daud, uitwao Bethlehemu, kwa kuwa yeye wa nyumba na jamaa ya Daud,

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

4 Yosefu pia alifanya safari kutoka mjini Nazareti mkoani Galilaya, na kwa vile alikuwa wa jamaa na ukoo wa Daudi, alikwenda mjini Bethlehemu mkoani Yudea, alikozaliwa mfalme Daudi.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

4 Yosefu pia alifanya safari kutoka mjini Nazareti mkoani Galilaya, na kwa vile alikuwa wa jamaa na ukoo wa Daudi, alikwenda mjini Bethlehemu mkoani Yudea, alikozaliwa mfalme Daudi.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

4 Yosefu pia alifanya safari kutoka mjini Nazareti mkoani Galilaya, na kwa vile alikuwa wa jamaa na ukoo wa Daudi, alikwenda mjini Bethlehemu mkoani Yudea, alikozaliwa mfalme Daudi.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

4 Hivyo Yusufu akapanda kutoka mji wa Nasiri ulioko Galilaya kwenda Yudea, hadi Bethlehemu, mji wa Daudi, kwa sababu yeye alikuwa wa ukoo na wa nyumba ya Daudi.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

4 Hivyo Yusufu akapanda kutoka mji wa Nasiri ulioko Galilaya kwenda Uyahudi, mpaka Bethlehemu, mji wa Daudi, kwa sababu yeye alikuwa wa ukoo na wa nyumba ya Daudi.

Tazama sura Nakili

Luka 2:4
24 Marejeleo ya Msalaba  

Alipokuwa akifikiri haya, malaika wa Bwana akamtokea katika udoto, akisema, Yusuf, mwana wa Daud, usikhofu kumchukua Mariamu mke wako, maana mimba yake ni kwa uweza wa Roho Mtakatifu.

akaenda, akakaa mji uliokwitwa Nazareti: illi litimie neno lililonenwa na manabii, Atakwitwa Mnazorayo.

Watu wote wakashika njia kwenda kuandikwa, killa mtu mjini kwake.

illi aandikwe pamoja na Mariamu mkewe ambae ameposwa nae; nae ana mimba.

Akaenda Nazareti, mahali alipokuwa amelelewa: akaingia katika sunagogi siku ya sabato, kama ilivyokuwa desturi yake, akasimama illi asome.

Nathanaeli akamwambia, Chaweza kitu chema kutoka Nazareti? Filipo akamwambia, Njoo uone.

Andiko halikusema ya kwamba Kristo atoka katika uzao wa Daud, na kutoka Bethlehemu, kijiji kile alichokaa Daud?

Tufuate:

Matangazo

Matangazo