Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Luka 2:34 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

34 Sumeon akawabariki, akamwambia Mariamu, mama yake, Hakika huyu amewekwa, waanguke, wasimame wengi katika Israeli; awe ishara inenwayo;

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

34 Simeoni akawabariki, akamwambia Maria mama yake, “Mtoto huyu atakuwa sababu ya kupotea na kuokoka kwa watu wengi katika Israeli. Naye atakuwa ishara itakayopingwa na watu;

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

34 Simeoni akawabariki, akamwambia Maria mama yake, “Mtoto huyu atakuwa sababu ya kupotea na kuokoka kwa watu wengi katika Israeli. Naye atakuwa ishara itakayopingwa na watu;

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

34 Simeoni akawabariki, akamwambia Maria mama yake, “Mtoto huyu atakuwa sababu ya kupotea na kuokoka kwa watu wengi katika Israeli. Naye atakuwa ishara itakayopingwa na watu;

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

34 Kisha Simeoni akawabariki, akamwambia Mariamu mama yake, “Mtoto huyu amewekwa kwa makusudi ya kuanguka na kuinuka kwa wengi katika Israeli. Atakuwa ishara ambayo watu watanena dhidi yake,

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

34 Kisha Simeoni akawabariki, akamwambia Mariamu mama yake, “Mtoto huyu amewekwa kwa makusudi ya kuanguka na kuinuka kwa wengi katika Israeli. Atakuwa ishara ambayo watu watanena dhidi yake,

Tazama sura Nakili




Luka 2:34
38 Marejeleo ya Msalaba  

Mwana wa Adamu alikuja, akila na kunywa, wakanena, Mlafi huyu, na mnywa mvinyo, rafiki wa watoza ushuru na wenye dhambi! Na hekima imepewa haki na watoto wake.


Alipokuwa katika kusema na makutano, mama yake na ndugu zake walikuwa wakisimama nje, wakitaka kusema nae.


Nae aangukiae juu ya jiwe hili atavunjikavunjika: nae amhae litamwangukia, litampondaponda.


wakinena, Bwana, tumekumbuka kwamba yule mjanja alisema, alipokuwa hayi bado, Baada ya siku tatu nitafufuka.


hatta na wewe upanga utakupenya roho yako; illi yafumike mawazo ya mioyo mingi.


Maana killa atendae manyonge huichukia nuru, wala haji kwenye nuru, matendo yake yasikemewe;


Bassi kwa sababu hii Wayahudi wakazidi kutaka kumwua, kwa kuwa hakuivunja sabato tu, bali pamoja na haya alimwita Mungu Baba yake, akijifanya sawa na Mungu.


Bali Wayahudi, walipowaona makutano, wakajaa wivu, wakayabisha maneno yaliyonenwa na Paolo, wakibisha na kutukana.


na wasipowakuta, wakamkokota Yason na baadhi ya ndugu mbele ya wakubwa wa mji, wakipiga kelele, wakisema, Watu hawa walioupindua ulimwengu wamefika na huku,


Kwa maana tamemwona mtu huyu mkorofi, muanzishaji wa fitina katika Mayahudi waliomo duniani, tena ni kichwa cha uzushi wa Wanazorayo.


Lakini tunataka kusikia kwako uonavyo wewe; kwa maana katika khabari za madhehebu hiyo tumekwisha kujua kwamba inanenwa vibaya kilia mahali.


Wafalme wa dunia wamejipanga, Na wakuu wamefanya shauri pamoja, Juu ya Bwana na juu ya Kristo wake.


Nenu la Mungu likaenea: hesahu ya wanafunzi ikazidi sana katika Yerusalemi: jamii kubwa la makuhani wakaitii Imani.


Kwa sababu gani? Kwa sababu hawakuitafuta kwa njia ya imani bali kana kwamba kwa njia ya matendo. Wakajikwaa juu ya jiwe lile likwaazalo,


bali sisi tunamkhubiri Kristo, aliyesulibiwa; kwa Wayahudi ni kikwazo, na kwa Wayunani ni upumbavu,


KWA maana Meikizedeki huyo, mfalme wa Salemi, kuhani wa Mungu aliye juu, aliyekutana na Ibrahimu baada ya kuwapiga wafalme, alimbariki;


Na haikanushiki kwamba mdogo hubarikiwa na mkubwa.


Mkilaumiwa kwa ajili ya jina la Kristo ni kheri yenu, kwa kuwa Roho ya utukufu na ya Mungu unawakalia; kwa hawo anatukanwa, bali kwenu ninyi anatukuzwa.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo