Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Luka 2:25 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

25 Bassi kulikuwako mtu katika Yerusalemi, jina lake Sumeon; na yule mtu mwenye haki, mtawa, akitazamia faraja ya Israeli: na Roho Mtakatifu alikuwa pamoja nae.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

25 Wakati huo huko Yerusalemu kulikuwa na mtu mmoja, mwema na mcha Mungu, jina lake Simeoni. Yeye alikuwa akitazamia kwa hamu ukombozi wa Israeli. Roho Mtakatifu alikuwa pamoja naye.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

25 Wakati huo huko Yerusalemu kulikuwa na mtu mmoja, mwema na mcha Mungu, jina lake Simeoni. Yeye alikuwa akitazamia kwa hamu ukombozi wa Israeli. Roho Mtakatifu alikuwa pamoja naye.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

25 Wakati huo huko Yerusalemu kulikuwa na mtu mmoja, mwema na mcha Mungu, jina lake Simeoni. Yeye alikuwa akitazamia kwa hamu ukombozi wa Israeli. Roho Mtakatifu alikuwa pamoja naye.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

25 Basi huko Yerusalemu kulikuwa mtu mmoja aliyeitwa Simeoni, aliyekuwa mwenye haki na mcha Mungu. Alikuwa akitazamia faraja ya Israeli, na Roho Mtakatifu wa Mungu alikuwa juu yake.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

25 Basi alikuwako huko Yerusalemu mtu mmoja jina lake Simeoni, ambaye alikuwa mwenye haki na mcha Mungu, akitarajia faraja ya Israeli, na Roho wa Mwenyezi Mungu alikuwa juu yake.

Tazama sura Nakili




Luka 2:25
22 Marejeleo ya Msalaba  

akaenda Yusuf, mtii wa Arimathaya, mstahiki, mtu wa baraza la mashauri, nae mwenyewe anautazamia ufalme wa Mungu; akafanya ujasiri, akaingia mbele ya Pilato akauomba mwili wake Yesu.


Ikawa Elizabeti alipoisikia salamu ya Mariamu, mtoto mchanga akaruka ndani ya tumbo lake; Elizabeti akajazwa Roho Mtakatifu, akapaaza sauti yake kwa nguvu, akasema,


Nao wote wawili wenye haki mbele ya Mungu, wakiendelea katika amri zote za Bwana na hukumu zake zote bila lawama.


Zakaria babae akajazwa Roho Mtakatifu, akatabiri, akinena,


Akitokea yeye nae saa ileile, alimshukuru Mungu, akawapasha khabari zake watu wote waliokuwa wakitazamia ukombozi katika Yerusalemi.


(mtu huyu hakuwa akikubali shauri lao wala tendo lao), mwenyeji wa Arimathaya, mji wa Wayahudi, nae mwenyewe akiutazamia ufalme wa Mungu.


mtu nitawa, mcha Mungu, yeye na nyumba yake yote, nae alikuwa akiwapa watu sadaka nyingi, na kumwomba Mungu siku zote.


Wakasema, Kornelio akida, mtu mwenye haki, mcha Mungu, aliye na sifa njema kwa taifa lote la Wayahudi, alionywa na malaika mtakatifu kutuma watu kwako, uende nyumbani kwake, apate kusikiliza maneno yako.


Na walikuwako Yerusalemi Wayahudi wakikaa, watu watawa, watu wa killa taifa chini ya uwingu.


Nami ninajizoeza katika neno hili kuwa na dhamiri isiyo na khatiya mbele ya Mungu na mbele ya watu.


Maana unabii haukuletwa zamani kwa mapenzi ya mwana Adamu; hali wana Adamu, watakatifu wa Mungu, walinena, wakiongozwa na Roho Mtakatifu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo