Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -

Luka 19:8 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

8 Zakkayo akasimama, akamwambia Bwana, Bwana, nussu ya mali zangu ninawapa maskini; na kama nimetoza mtu kitu kwa kumsingizia uwongo ninamrudishia marra nne.

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

8 Lakini Zakayo akasimama, akamwambia Yesu, “Sikiliza Bwana! Mimi nitawapa maskini nusu ya mali yangu, na kama nimenyanganya mtu yeyote kitu, nitamrudishia mara nne.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

8 Lakini Zakayo akasimama, akamwambia Yesu, “Sikiliza Bwana! Mimi nitawapa maskini nusu ya mali yangu, na kama nimenyanganya mtu yeyote kitu, nitamrudishia mara nne.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

8 Lakini Zakayo akasimama, akamwambia Yesu, “Sikiliza Bwana! Mimi nitawapa maskini nusu ya mali yangu, na kama nimenyang'anya mtu yeyote kitu, nitamrudishia mara nne.”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

8 Lakini Zakayo akasimama na kumwambia Bwana Isa, “Tazama, Bwana! Sasa hivi nusu ya mali yangu ninawapa maskini, nami kama nimemdhulumu mtu yeyote kitu chochote, nitamrudishia mara nne ya hicho kiwango.”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

8 Lakini Zakayo akasimama na kumwambia Bwana Isa, “Tazama, Bwana! Sasa hivi nusu ya mali yangu ninawapa maskini, nami kama nimemdhulumu mtu yeyote kitu chochote, nitamrudishia mara nne ya hicho kiwango.”

Tazama sura Nakili

Luka 19:8
22 Marejeleo ya Msalaba  

Lakini toeni sadaka vile vya ndani, na tazama, vitu vyote ni safi kwemi.

Viuzeni mlivyo navyo, katoeni sadaka, jifanyieni mifuko isiyochakaa, akiba isiyopungua katika mbingu, asikokaribia mwizi, wala nondo kuharibu.

Na mimi nawaambia ninyi, Jifanyieni rafiki kwa mamona ya udhalimu, illi itakapopunguka wawakaribishe ninyi katika makao ya milele.

Hatta watu walipoona wakanungʼunika wote, wakisema, ya kama, Ameingia akae kwa mtu mwenye dhambi.

Na Bwana alipomwona, akamhurumia, akamwambia, Usilie.

Yohana akaita wawili katika wanafunzi wake akawapeleka kwa Yesu, akisema, Wewe ndiye yule ajae, au tumtazamie mwingine?

Tufuate:

Matangazo

Matangazo