Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -

Luka 19:37 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

37 Hatta alipokuwa amekwisha kukaribia matelemko va mlima wa mizeituni, kundi lote la wanafunzi wake wakaanza kufurahi na kumhimidi Mungu kwa sauti kuu, kwa ajili ya miujiza yote waliyoiona,

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

37 Alipofika karibu na Yerusalemu, katika mteremko wa mlima wa Mizeituni, umati wote na wanafunzi wake wakaanza kushangilia na kumtukuza Mungu kwa sauti kubwa kwa sababu ya mambo makuu waliyoyaona;

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

37 Alipofika karibu na Yerusalemu, katika mteremko wa mlima wa Mizeituni, umati wote na wanafunzi wake wakaanza kushangilia na kumtukuza Mungu kwa sauti kubwa kwa sababu ya mambo makuu waliyoyaona;

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

37 Alipofika karibu na Yerusalemu, katika mteremko wa mlima wa Mizeituni, umati wote na wanafunzi wake wakaanza kushangilia na kumtukuza Mungu kwa sauti kubwa kwa sababu ya mambo makuu waliyoyaona;

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

37 Alipokaribia mahali yanapoanzia miteremko ya Mlima wa Mizeituni, umati wote wa wafuasi wake wakaanza kumsifu Mungu kwa furaha kwa sauti kuu kwa ajili ya matendo yote ya miujiza waliyoyaona. Wakasema:

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

37 Alipokaribia mahali yanapoanzia materemko ya Mlima wa Mizeituni, umati wote wa wafuasi wake wakaanza kumsifu Mungu kwa furaha kwa sauti kuu kwa ajili ya matendo yote ya miujiza waliyoyaona. Wakasema:

Tazama sura Nakili

Luka 19:37
20 Marejeleo ya Msalaba  

HATTA walipokaribia Yerusalemi, na kufika Bethfage, katika mlima wa Mizeituni, ndipo Yesu akatuma wanafunzi wawili,

Hatta alipokuwa ameketi katika mlima wa mizeituni, kuelekea hekalu, Petro, na Yakobo, na Yohana, na Andrea wakamwuliza kwa faragha, Tuambie, haya yatakuwa lini?

Wakiisha kuimba wakatoka kwenda mlima wa mizeituni.

Marra akapata kuona, akamfuata, akimtukuza Mungu; na watu wote walipoona wakampa Mungu sifa.

Akaja mwingine akasema, Bwana, tazama, mane yako hii niliyokuwa nayo, imewekwa akiba katika leso:

Hatta alipokaribia Bethfage na Bethania karibu ya mlima wa mizeituni, akatuma wawili katika wanafunzi wake, akisema,

Nae alipokuwa akienda, wakatandaza nguo zao njiani.

Khofu ikawashika wote, wakamtukuza Mungu, wakisema, Nabii mkuu ametokea kwetu: na Mungu amewajilia watu wake.

Kwa sababu hiyo makutano wakaenda kumlaki, kwa sababu wamesikia ya kwamba amefanya ishara hii.

Tufuate:

Matangazo

Matangazo