Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Luka 18:43 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

43 Marra akapata kuona, akamfuata, akimtukuza Mungu; na watu wote walipoona wakampa Mungu sifa.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

43 Na mara huyo kipofu akapata kuona, akamfuata Yesu akimtukuza Mungu. Watu wote walipoona hayo, wakamsifu Mungu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

43 Na mara huyo kipofu akapata kuona, akamfuata Yesu akimtukuza Mungu. Watu wote walipoona hayo, wakamsifu Mungu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

43 Na mara huyo kipofu akapata kuona, akamfuata Yesu akimtukuza Mungu. Watu wote walipoona hayo, wakamsifu Mungu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

43 Akapata kuona mara hiyo, akamfuata Isa, huku akimsifu Mungu. Watu wote walipoona mambo hayo, nao wakamsifu Mungu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

43 Akapata kuona saa ile ile, akamfuata Isa, huku akimsifu Mwenyezi Mungu. Watu wote walipoona mambo hayo, nao wakamsifu Mungu.

Tazama sura Nakili




Luka 18:43
30 Marejeleo ya Msalaba  

vipofu wanapata kuona, viwete wanatembea, wenye ukoma wanatakasika, viziwi wanasikia, wafu wanafufuliwa, na maskini wanakhubiriwa khabari njema.


Vipofu na viwete wakamwendea hekaluni, akawaponya.


Makutano wakimwona, wakastaajabu, wakamtukuza Mungu, aliyewapa watu mamlaka ya jinsi hii.


Na aliposema haya, watu wote walioshindana nae wakatahayarika, mkutano wote wakafurahi kwa ajili ya mambo matukufu yaliyotendwa nae.


Hatta alipokuwa amekwisha kukaribia matelemko va mlima wa mizeituni, kundi lote la wanafunzi wake wakaanza kufurahi na kumhimidi Mungu kwa sauti kuu, kwa ajili ya miujiza yote waliyoiona,


Akasimama karibu nae akaikemea ile homa, ikamwacha; marra akaondoka akawakhudumu.


Ushangao ukawashika wote wakamtukuza Mungu: wakajaa khofu, wakinena, Tumeona maajabu leo.


Watu wote wakashangaa kwa adhama yake Mungu. Hatta wote walipokuwa wakistaajabia mambo yote aliyoyafanya akawaambia wanafunzi wake,


Waliposikia maneno haya wakanyamaza, wakamtukuza Mungu, wakisema, Bassi, Mungu amewajalia mataifa nao toba liletalo uzima.


uwafumhue macho yao, waiache giza na kuielekea nuru, na waziache nguvu za Shetani na kumwelekea Mungu, na wapate masamaha ya dhambi zao, na urithi miongoni mwao waliotakaswa kwa imani iliyo kwangu.


Nao walipokwisha kuwaogofya tena wakawafungua, wasione njia ya kuwaadhibu, kwa sababu ya watu: kwa kuwa watu wote walikuwa wakimtukuza Mungu kwa hayo yaliyotendeka:


Wakamtukuza Mungu kwa ajili yangu.


Bali ninyi m mzao mteule, ukubani wa kifaume, taifa takatifu, watu wa milki, mpate kutangaza fadhili zake aliyewaita mtoke gizani mkaingie katika nuru yake ya ajabu;


Tufuate:

Matangazo


Matangazo