Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -

Luka 18:13 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

13 Na yule mtoza ushuru akasimama mbali, asitake hatta kuinua macho yake mbinguni; hali akajipigapiga kifua, akisema, Mungu, uniwie radhi mimi mwenye dhambi.

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

13 Lakini yule mtozaushuru, akiwa amesimama kwa mbali bila hata kuinua macho yake mbinguni, ila tu akijipiga kifua kwa huzuni, alisema: ‘Ee Mungu, unionee huruma mimi mwenye dhambi.’

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

13 Lakini yule mtozaushuru, akiwa amesimama kwa mbali bila hata kuinua macho yake mbinguni, ila tu akijipiga kifua kwa huzuni, alisema: ‘Ee Mungu, unionee huruma mimi mwenye dhambi.’

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

13 Lakini yule mtozaushuru, akiwa amesimama kwa mbali bila hata kuinua macho yake mbinguni, ila tu akijipiga kifua kwa huzuni, alisema: ‘Ee Mungu, unionee huruma mimi mwenye dhambi.’

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

13 “Lakini yule mtoza ushuru akasimama mbali, wala hakuthubutu hata kuinua uso wake kutazama mbinguni, bali alijipigapiga kifuani na kusema: ‘Mungu, nihurumie, mimi mwenye dhambi.’

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

13 “Lakini yule mtoza ushuru akasimama mbali, wala hakuthubutu hata kuinua uso wake kutazama mbinguni, bali alijipigapiga kifuani na kusema: ‘Mungu, nihurumie, mimi mwenye dhambi.’

Tazama sura Nakili

Luka 18:13
45 Marejeleo ya Msalaba  

Filipo, na Bartolomayo, na Tomaso, na Mattayo mtoza ushuru; Yakobo wa Alfayo, na Lebbayo, aliyekwitwa Thaddayo;

Tena usalipo, usiwe kama wanafiki: kwa maana wapenda kusali wakisimama katika sunagogi na katika pembe za njia, illi waonekane na watu. Amin, nawaambieni, Wamekwisha kupata thawabu yao.

Lakini shikeni njia, mkajifunze maana yake maneno haya, Nataka rehema, wala si sadaka: kwa maana sikuja kuwaita wenye haki, bali wenye dhambi wapate kutubu.

Nanyi, killa msimamapo na kusali, sameheni, kama mkiwa na neno juu ya mtu: illi Baba yenu aliye mbinguni awasamehe na ninyi makosa yenu.

Alipokuwa akiingia kijiji kimoja, wakakutana nae watu kumi wenye ukoma, waliosimama mbali;

Akiisha akajitenga nao kadiri ya mtupo wa jiwe, akapiga magoti, akaomba, akisema,

Na makutano wote waliokusanyika kutazama haya, walipotazama yaliyofanyika, wakarudi, wakijipiga vifua.

Simon Petro alipoona haya, akaanguka magotini pa Yesu, akasema, Toka kwangu, kwa sababu mimi ni mtu mwenye dhambi, Bwana.

Walipoyasikia haya wakachomwa mioyo yao, wakamwambia Petro na mitume wengine, Tutendeje, ndugu zetu?

Bali Mungu aonyesha pendo lake kwetu, kwa kuwa Kristo alikufa kwa ajili yetu, tulipokuwa tungali wenye dhambi.

Maana, angalieni, kuhuzunishwa kuko huko mbele za Mungu kwalitenda bidii ya namna gani ndani yenu; naam, na kujitetea, naam, na kukasirika, naam, na khofu, naam, na shauku, naam, na kujitahidi, naam, na kisasi. Kwa killa njia mmejionyesha kuwa safi katika jambo hilo.

Ni neno la kuaminiwa, listahililo kukubaliwa na watu wote, ya kwamba Kristo Yesu alikuja ulimwenguni, awaokoe wenye dhambi; na mimi wa kwanza wao.

Bassi na tukikaribie kiti cha neema kwa nthubuitifu, illi tupewe rehema, na kupata neema ya kutusaidia wakati wa mahitaji.

Kwa sababu nitawasamehe dhumlumu zao, na dhambi zao sitazikumbuka tena.

Tufuate:

Matangazo

Matangazo