Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Luka 17:6 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

6 Bwana akasema, Mkiwa na imani kama punje ya kharadali, mngeuambia mzambarau huu, Ngʼoka ukapandwe baharini, nao ungewatiini.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

6 Naye Bwana akajibu, “Kama imani yenu ingekuwa ndogo hata kama chembe ndogo ya haradali, mngeweza kuuambia mti huu wa mkuyu: ‘Ngoka ukajipandikize baharini,’ nao ungewatii.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

6 Naye Bwana akajibu, “Kama imani yenu ingekuwa ndogo hata kama chembe ndogo ya haradali, mngeweza kuuambia mti huu wa mkuyu: ‘Ngoka ukajipandikize baharini,’ nao ungewatii.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

6 Naye Bwana akajibu, “Kama imani yenu ingekuwa ndogo hata kama chembe ndogo ya haradali, mngeweza kuuambia mti huu wa mkuyu: ‘Ng'oka ukajipandikize baharini,’ nao ungewatii.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

6 Bwana akawajibu, “Kama mngekuwa na imani ndogo kama punje ya haradali, mngeweza kuuambia mti huu wa mkuyu, ‘Ng’oka ukaote baharini,’ nao ungewatii.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

6 Bwana Isa akawajibu, “Kama mkiwa na imani ndogo kama punje ya haradali, mngeweza kuuambia mti huu wa mkuyu, ‘Ng’oka ukaote baharini,’ nao ungewatii.

Tazama sura Nakili




Luka 17:6
13 Marejeleo ya Msalaba  

Akasema, Njoo. Petro akashuka chomboni, akatembea juu ya maji, illi kumwendea Yesu.


Yesu akawaambia, Kwa sababu ya kutokuamini kwenu. Kwa maana, amin, nawaambieni, Mkiwa na imani kama punje ya kharadali mtauambia mlima huu, Ondoka hapa hatta kule; nao utaondoka; wala halitakuwako neno lisilowezekana kwenu.


Yesu akajibu, akawaambia, Amin, nawaambieni, Mkiwa na imani, msipokuwa na shaka, mtafanya si hilo la mtini tu, lakini hatta mkiuambia mlima huu, Ngʼoka, ukatupwe baharini, itatendeka.


Ni kama punje ya kharadali ambayo, ipandwapo katika inchi, ni ndogo kuliko mbegu zote zilizo katika inchi,


Yesu akamwambia, Ukiweza kuamini: yote yawezekana kwake aaminiye.


Umefanana na punje ya kharadali, aliyotwaa mtu akaitupa katika shamba lake, ikakua, ikawa mti mkubwa, ndege za anga wakatua katika matawi yake.


Lakini nani kwenu mwenye mtumishi anaelima, an anaeehunga kondoo? je! amwambia marra atakapoingia, akitoka mashamba, Njoo upesi, keti, ule chakula?


Akatangulia mbio, akapanda juu ya mkuyu apate kumwona, kwa sababu alitaka kupita njia ile.


Na Bwana alipomwona, akamhurumia, akamwambia, Usilie.


Yohana akaita wawili katika wanafunzi wake akawapeleka kwa Yesu, akisema, Wewe ndiye yule ajae, au tumtazamie mwingine?


Tena nijapokuwa na unabii, na kujua siri zote na maarifa yote, nijapokuwa na imani timilifu kiasi cha kuweza kuhamisha milima, kama simi upendo, si kitu mimi.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo