Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Luka 17:24 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

24 Kwa maana kama vile umeme umulikavyo toka upande huu chini ya mbingu hatta upande huu chini ya mbingu, ndivyo na Mwana wa Adamu atakavyokuwa katika siku yake.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

24 Kwa maana kama vile umeme unavyotokea ghafla na kuangaza anga upande mmoja hadi mwingine, ndivyo Mwana wa Mtu atakavyokuwa siku ile yake.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

24 Kwa maana kama vile umeme unavyotokea ghafla na kuangaza anga upande mmoja hadi mwingine, ndivyo Mwana wa Mtu atakavyokuwa siku ile yake.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

24 Kwa maana kama vile umeme unavyotokea ghafla na kuangaza anga upande mmoja hadi mwingine, ndivyo Mwana wa Mtu atakavyokuwa siku ile yake.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

24 Kwa maana kama vile radi imulikavyo katika anga kuanzia mwisho mmoja hadi mwingine, ndivyo atakavyokuwa Mwana wa Adamu katika siku yake.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

24 Kwa maana kama vile umeme wa radi umulikavyo katika anga kuanzia mwisho mmoja hadi mwingine, ndivyo atakavyokuwa Mwana wa Adamu katika siku yake.

Tazama sura Nakili




Luka 17:24
16 Marejeleo ya Msalaba  

Kwa maana kama vile umeme utokavyo mashariki ukaonekana hatta magharibi; hivyo ndivyo kutakavyokuwa kuja kwake Mwana wa Adamu.


ndipo itakapoonekana ishara yake Mwana wa Adamu mbinguni: ndipo mataifa yote ya ulimwengu wataomboleza, nao watamwona Mwana wa Adamu akija juu ya mawingu ya mbingu kwa nguvu pamoja na utukufu mwingi.


Hatta atakapokuja Mwana wa Adamu katika utukufu wake, na malaika watakatifu wote pamoja nae, ndipo atakapoketi katika kiti cha utukufu wake:


Yesu akamwambia. Wewe umesema: lakini nawaambieni, Tangu sasa mtamwoua Mwana wa Adamu ameketi mkono wa kuume wa nguvu, akija juu ya mawingu.


Wala watu hawawashi taa na kuiweka chini ya kibaba, bali juu ya kibao cha kuwekea taa; nayo yaangaza wote waliomo nyumbani.


na yeye atawathubutisheni hatta mwisho, msilaumiwe siku ile ya Bwana wetu Yesu Kristo.


Maana ninyi wenyewe mnajua yakini ya kuwa siku ya Bwana yaja kama vile mwizi ajavyo usiku.


msifadhaishwe upesi na kuaeha nia yenu, wala msistushwe, kwa roho wala kwa neno, wala kwa waraka unaodhaniwa kuwa ni wetu, ya kwamba siku ya Bwana imekwisha kuwapo.


Hapo ndipo atakapofunuliwa yule asi, ambae Bwana Yesu atamwua kwa pumzi ya kinywa chake, na kumwangamiza kwa mafunuo ya kuwako kwake;


Bassi, na ninyi subirini, jithubutisheni mioyo yenu, kwa maana kuja kwake Bwana kunakaribia.


Maana siku ya Bwana itakuja kama mwizi usiku; katika siku biyo mbingu zitatoweka kwa mshindo mkuu, na viumbe vya asili vitaunguzwa, na kufumuliwa, na inchi na kazi zilizomo ndani yake zitateketea.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo