Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Luka 17:16 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

16 akaanguka kufudifudi miguuni pake, akimshukuru; nae ni Msamaria.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

16 Akajitupa chini mbele ya miguu ya Yesu huku akimshukuru. Huyo alikuwa Msamaria.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

16 Akajitupa chini mbele ya miguu ya Yesu huku akimshukuru. Huyo alikuwa Msamaria.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

16 Akajitupa chini mbele ya miguu ya Yesu huku akimshukuru. Huyo alikuwa Msamaria.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

16 Akajitupa miguuni mwa Isa akamshukuru. Yeye alikuwa Msamaria.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

16 Akajitupa miguuni mwa Isa akamshukuru. Yeye alikuwa Msamaria.

Tazama sura Nakili




Luka 17:16
21 Marejeleo ya Msalaba  

Hawa thenashara Yesu aliwatuma, akawaagiza, akinena, Katika njia ya Mataifa msiende, wala mjini mwa Wasamaria msiingie:


Wakaingia nyumbani, wakamwona mtoto pamoja na Mariamu mama yake, wakaanguka wakasujudu; nao walipokwisha kufungua hazina zao, wakamtolea tumi, dhahabu, uvumba, na manemane.


Na yule mwanamke akaingiwa na khofu na kutetemeka, akijua lililompata, akaja akamwangukia, akamweleza kweli yote.


Yesu akajiliu, akasema, Si wote kumi waliotakasika? Wale tissa wa wapi?


Simon Petro alipoona haya, akaanguka magotini pa Yesu, akasema, Toka kwangu, kwa sababu mimi ni mtu mwenye dhambi, Bwana.


Bassi yule mwanamke wa Kisamaria akamwambia, Imekuwaje wewe Myahudi kutaka maji kwangu, nami ni mwanamke wa Kisamaria? kwa maana Wayahudi hawachangamani na Wasamaria.


illi wote wamheshimu Mwana kama wanavyomheshimu Baba. Asiyemheshimu Mwana, hamheshimu Baba aliyempeleka.


Wayahudi wakajibu wakamwambia, Hatuneni vema sisi kwamba wewe u Msamaria, na una pepo?


Lakini mtapokea nguvu, akiisha kuwajilia Roho Mtakatifu; nanyi mtakuwa mashahidi wangu katika Yerusalemi, na katika Yahudi yote, na Samaria, na hatta mwisho wa inchi.


na hivyo siri za moyo wake huwa wazi; na hivyo, akianguka kifudifudi, atamwabudu Mungu, akikiri ya kuwa Mungu yu kati yenu hila shaka.


Nikaanguka mbele ya miguu yake, nimsujudie, akaniambia, Angalia, usifanye hivi: mimi mjoli wako na mmoja wa ndugu zako walio na ushuhuda wa Yesu. Msujudu Mungu: kwa maana ushuhuda wa Yesu ni roho ya unabii.


ndipo hawa wazee ishirini na wane watakapoanguka mbele zake aketiye juu ya kiti cha enzi, nao watamsujudu veye aliye hayi hatta milele na milele, nao watatupa taji zao mbele ya kiti eha enzi, wakisema,


Na wale nyama wane wenye uhayi wakasema, Amin. Na wale wazee ishirini na wane wakaanguka wakamsujudu yeye aliye hayi milele na milele.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo