Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Luka 16:9 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

9 Na mimi nawaambia ninyi, Jifanyieni rafiki kwa mamona ya udhalimu, illi itakapopunguka wawakaribishe ninyi katika makao ya milele.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

9 Naye Yesu akaendelea kusema, “Nami nawaambieni, jifanyieni marafiki kutokana na mali ya dunia, ili zitakapowaishieni, wawapokeeni katika makao ya milele.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

9 Naye Yesu akaendelea kusema, “Nami nawaambieni, jifanyieni marafiki kutokana na mali ya dunia, ili zitakapowaishieni, wawapokeeni katika makao ya milele.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

9 Naye Yesu akaendelea kusema, “Nami nawaambieni, jifanyieni marafiki kutokana na mali ya dunia, ili zitakapowaishieni, wawapokeeni katika makao ya milele.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

9 Nawaambia, tumieni mali ya dunia kujipatia rafiki, ili itakapokwisha, mkaribishwe katika makao ya milele.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

9 Nawaambia, tumieni mali ya kidunia kujipatia marafiki, ili itakapokwisha, mkaribishwe katika makao ya milele.

Tazama sura Nakili




Luka 16:9
28 Marejeleo ya Msalaba  

Yesu akamwambia, Ukitaka kuwa mkamilifu, enenda ukauze mali zako, uwape maskini, nawe utakuwa na hazina mbinguni; kiisha njoo unifuate.


Msijiwekee hazina duniani, nondo na kutu ziharibupo, na wevi huvunja na kuiba:


Hakuna mtu awezae kuwatumikia bwana wawili; kwa maana atamchukia mmoja, na kumpenda wa pili; au atamshika mmoja, na kumtweza wa pili. Hamwezi kumtumikia Mungu na mamona.


Lakini toeni sadaka vile vya ndani, na tazama, vitu vyote ni safi kwemi.


Viuzeni mlivyo navyo, katoeni sadaka, jifanyieni mifuko isiyochakaa, akiba isiyopungua katika mbingu, asikokaribia mwizi, wala nondo kuharibu.


kwa sababu hawana kitu cha kukulipa; maana utalipwa katika ufufuo wa wenye haki.


Bassi, ikiwa hamkuwa waaminifu katika mamona ya udhalimu, nani atakaewaaminisheni mali ya kweli?


Hakuna mtumishi awezae kuwatumikia bwana wawili: maana au atamchukia huyu, na kumpenda huyu; ama atashikamana na huyu, na kumdharau huyu. Hamwezi kumtumikia Mungu na Mamona.


Nimekwisha kujua nitakalotenda, illi, nitolewapo katika nwakili, wanikaribishe nyumbani mwao.


Kornelio, maombi yako yamesikiwa, na sadaka zako zinakumbukwa mbele za Mungu.


Akamtazama sana, akaogopa akasema, Kuna nini, Bwana? Akamwambia, Maombi yako na sadaka zako zimefika juu na kuwa ukumbusho mbele za Mungu.


Maana mateso mepesi yetu, yaliyo ya muda wa kitambo tu, yatufanyia utukufu wa milele ulio mwingi sana zaidi;


jilindeni katika upendo wa Mungu, mkingojea rehema ya Bwana wetu Yesu Krislo, hatta mpate uzima wa milele.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo