Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -

Luka 16:25 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

25 Ibrahimu akasema, Mwanangu, kumbuka ya kuwa ulipokea mema yako katika maisha yako, na Lazaro kadhalika mabaya; lakini sasa yeye yupo hapa anafarajiwa, nawe unanmizwa.

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

25 Lakini Abrahamu akamjibu: ‘Kumbuka mwanangu kwamba ulipokea mema yako katika maisha, naye Lazaro akapokea mabaya. Sasa lakini, yeye anatulizwa, nawe unateswa.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

25 Lakini Abrahamu akamjibu: ‘Kumbuka mwanangu kwamba ulipokea mema yako katika maisha, naye Lazaro akapokea mabaya. Sasa lakini, yeye anatulizwa, nawe unateswa.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

25 Lakini Abrahamu akamjibu: ‘Kumbuka mwanangu kwamba ulipokea mema yako katika maisha, naye Lazaro akapokea mabaya. Sasa lakini, yeye anatulizwa, nawe unateswa.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

25 “Lakini Ibrahimu akamjibu, ‘Mwanangu, kumbuka kwamba wakati wa uhai wako ulipata mambo mazuri, lakini Lazaro alipata mambo mabaya. Lakini sasa anafarijiwa hapa na wewe uko katika maumivu makuu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

25 “Lakini Ibrahimu akamjibu, ‘Mwanangu, kumbuka kwamba wakati wa uhai wako ulipata mambo mazuri, lakini Lazaro alipata mambo mabaya. Lakini sasa anafarijiwa hapa na wewe uko katika maumivu makuu.

Tazama sura Nakili

Luka 16:25
25 Marejeleo ya Msalaba  

wakinena, Bwana, tumekumbuka kwamba yule mjanja alisema, alipokuwa hayi bado, Baada ya siku tatu nitafufuka.

Na mguu wako ukikukosesha, ukate: ni kheri kuingia katika uzima, umepungukiwa mguu, kuliko kuwa na miguu miwili, na kutupwa katika jebannum, katika moto usiozimika;

Na maskini mmoja, jina lake Lazaro, hutupwa mlangoni pake, ana vidonda,

Bassi katika akhera akainua macho yake, akiwa katika adhabu, akamwona Ibrahimu yuko mbali, na Lazaro kifuani pake.

Na zaidi ya haya yote, kati yetu sisi na ninyi lipo shimo kuhwa limewekwa, hatta watu watakao kutoka huku wasiweze kuja kwenu, wala wale wa huko wasivuke kuja kwetu.

Bali ole wemi ninyi mlio na mali: kwa sababu mmekwisha kuwa na faraja yenu.

Haya nimewaambieni, mpate kuwa na amani ndani yangu. Ulimwenguni mtapata shidda: lakini jipeni moyo; mimi nimeushinda ulimwengu.

wakifanya imara roho za wanafunzi na kuwaonya wakae katika imani, na ya kwamba imetupasa kuingia katika ufalme wa Mungu kwa njia ya shidda nyingi.

Kwa kuwa ile nia ya mwili ni uadui juu ya Mungu, kwa maana haitii sharia ya Mungu wala haiwezi.

mwisho wao uharibifu, mungu wao tumbo, utukufu wao u katika aibu yao, waniao mambo ya duniani.

mtu asifadhaishwe na mateso haya: maana ninyi wenyewe mnajua ya kuwa twawekewa haya.

akaona ui afadhali kupata mateso pamoja na watu wa Mungu kuliko kujifurahisha kwa dhambi kitamho;

Msiipende dunia, wala mambo yaliyomo katika dunia. Mtu akiipenda dunia, kumpenda Baba hakumo ndani yake.

Nikamwambia, Bwana wangu, wajua wewe. Akaniambia, Hawo ndio wanaotoka katika shidda ile iliyo kuu, nao wamefua mavazi yao wakayafanya meupe katika damu ya Mwana Kondoo.

Tufuate:

Matangazo

Matangazo